Naomba ufafanuzi katika hili la mtoto kunywa juice ya nanasi na kutoa jasho jingi

Naomba ufafanuzi katika hili la mtoto kunywa juice ya nanasi na kutoa jasho jingi

Kibororoni

Member
Joined
Dec 19, 2019
Posts
77
Reaction score
154
Naamini mmesherehekea salama pumziko la pasaka na poleni kwa ambao haikuwa amani kwa namna moja au nyingine.

Aidha poleni kwa misukosuko na taaruki ya ugonjwa wa COVID -19 najua imeleta athari kadhaa zikiwemo vifo na makatazo ya kujumuika katika shughuli mbalimbali za mikusanyiko. Zaidi kwa ili tuendelee kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na wizara ya afya na wadau wengine.

Napenda kuuliza jambo moja linalonishangaza nikiamini nitapata majawabu kwani jukwaa hili limesheheni wataalamu kwenye weredi mkubwa kwa mambo ya afya.

Kwa ufupi ni kuwa nina mtoto wa miezi nane nikimpa juice ya nanasi anatoa jasho jingi sana. Akinywa maji anakuwa kawaida tu na pia akila chakula chakula pia anakuwa kawaida tu.
Naomba kueleweshwa juu ya nini kinachotokea na je kiafya juice ya nanasi inafaa kwa hali inayomtokea mtoto huu ili ikiwezekana niache kumpa juice hiyo?

Nawasilisha wataalam nikitaraji kupata ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom