Biashara ya hisa inakuaje?
CWT wanauza hisa na ninahitaji kununua ila sina elim ya biashara hii.
Okay Nisiwe Mchoyo..........
Tunaanza na Maana ya hisa (share).
Hisa ni vipande vidogo vidogo au cheti ambacho kinawakilisha umiliki wa kamapuni fulani. Hisa huwa zinatofautiana bei kutokana na kampuni inafanya shughuli gani na inapokelewaje Katika jamii.
MASOKO YA HISA.
Hisa unaweza kununua sehemu yoyote Duniani na baadhi ya masoko makubwa ni New York Stock Exchange (NYSE) Na London Stock Exchange (LSE). Hapa Tanzania tuna Secondary market ya hisa ambayo inaitwa Dar-es-salaam Stock Exchange (DSE) Ni moja kati ya Masoko Bora kabisa ya hisa Barani Afrika sina uhakika sana ila ina makampuni kama 21 hivi. Ambayo ni SIMBA,NMB,CRDB,TBL,TWIGA,MKOMBOZI bank,ACCASIA,TCC, na Mengineyo.....
HISA ZIPI MTU ANATAKIWA ANUNUE.
Malipo ya hisa yanategemea sana Shughuli katika soko na jamii tunayoishi hapo ndipo bei yake hupanda au kushuka. Mfano kampuni ya TBLmiaka mitatu nyuma hisa yake moja ilikua ikiuzwa hadi Tshs. 5000 lakini sasa hivi ipo kwenye Tshs.14,500 inapanda haraka sana hii inaonesha kuwa kampuni inafanya vizuri hivyo itakushawishi kununua hisa japo inahitaji Mtaji mkubwa...
Pia katika Mabenki Tunaona Benki ya N.M.B, CRDB na Mkombozi benki.Katika mambo ya Uwekezaji N.M.B iko vizuri zaidi ya CRDB. CRDB ina struggle sana hadi sasa inataka kuzidiwa hata na mkombozi bank ambayo imeanzishwa mwaka 2009 hisa zao walikua wakiuza Tshs. 300 lakini sasa hivi zipo kwenye 1200 wakati CRDB yenyewe ipo kwenye sh. 500 mara sh. 490 na kama nilivyosema awali bei ya hisa hupandishwa nashughuli katika soko kama hisa zinanunuliwa sana bei yake huongezeka na kama hazinunuliwi bei yake hudorora ambapo kwa mwekezeji unakuwa na hofu. Kwani kampuni yako inakua inafanya vibaya. Hivyo basi mwanahisa yoyote anapenda kuona hisa zikipanda bei ili apate Capital gain.
KIASI CHA UNUNUZI WA HISA / UWEKEZAJI
Hisa unazinunua kutokana na mtaji wako ulionao na kwenye makampuni Ukiwekeza Hela yako nyingi (ukinunua hisa nyingi) inamaanisha kuwa unamiliki kampuni kwa kiasi kikubwa hivyo unaweza kuwa kiongozi katika hiyo kampuni unaingia katika board of Directors na hapa unapata mshahara kwa mwezi.
FAIDA ZA HISA.
Hisa zinafaida za aina mbili yaani unaweza kupata gawio (Dividend) au ongezeko la mtaji (capital gain). Tunaanza na
Gawio hiki ni kiasi cha pesa ambacho huamuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ili kuwalipa wanahisha kutokana na Faida iliyopatiana kwa mwaka husika na hulipwa mara baada ya kulipa kodi (Corporate Tax 30%). Katika sheria ya Makapuni Companies Act ya mwaka 2002 haitoi ulazima wa kulipa gawio kwa wanahisa hivyo basi kulipwa gawio siyo lazima. Na hulipwa pale kampuni inapopata faida pia hiyo faida wanaweza kuilekezea kwenye mambo mengine ya uwekezaji.
Ongezeko la Mtaji Capital gain hii hutokea pale mwanahisa anapouza hisa zake. Mfano kama mwaka 2012 ulinunua hisa za TBL 500 Moja kwa Sh. 5,000 Sasa hivi 2015 unauza hisa za TBL 500 moja 1400 hapo kuna Capital gain ya Sh. 9000×500 =4.5Million ukijumlisha na Dividend unapata hela nyingi tuu kama uliwekeza mtaji mkubwa na mara nyingi hakunaga kodi.
Anayejua zaidi atujuze pia kama una swali uliza.