Naomba ufafanuzi kuhusu CVT Sport

Kama inawezekana, kaa mbali na CVT Transmission either nunua Standard/Manual au Automatic za kawaida.. CVT transmissions zinazingua kwa ujumla, zinavyozidi kuzeeka ndiyo matatizo huanza kujitokeza. Fanya utafiti wako mwenyewe utajionea.
Wewe unamshauri mwenzako akae mbali na CVT wakati Dunia ndio inaelekea huko?
 
Kwamba hio Rumion ina CVT?
Rumion ina CVT tu. Hakuna Rumion yenye gearbox ya aina nyingine.

Pia Rumion zimetengenezwa kuanzia 2007. Gari nyingi ambazo toyota ametengeneza kuanzia miaka hiyo amefunga CVT.
 
Hiyo Direct Shift Gearbox si ndiyo Dual Clutch Gearbox (DCG) hii inabalaa Sana ipo kwenye VW Golf na Skoda za miaka ya karibuni.
 
Kwamba hio Rumion ina CVT?
Yes....
Rumion inatumia CVT transmission
 
Duuu!!!
Technology inazidi kupaa siku Hadi siku Hadi siku ndiyo maana nchi kama America Kwa 83% wanatumia Magari ya automatic sasa Kwa style hii naona Magari ya manual transmission yataondoka sokoni moja Kwa moja.

Kwa mfano ambao umetoa hapo juu wa DSG TRANSMISSION naona ni ngumu tena Kwa manual transmission kurudi Kwenye soko
 
Yaani hiyo gearbox wanakuambia ni kama wameunganisha gearbox mbili za manual.

Moja inakuwa na gear za Odd 1, 3, 5,... Hii inaendeshwa na clutch moja.

Nyingine inakuwa na gear za Even 2, 4, 6,... Hii inaendeshwa na clutch nyingine.

Na sijaonaga DSG ambayo ina gear chini ya 6.

DSG zote zinaanzia gear 6, 7 mpaka 10.
 
Kwamba hio Rumion ina CVT?
Yes....
Toyota rumion inatumia CVT transmission
Shukrani Mkuu Kwa haya madini maana hii ni zaidi ya elimu hasa Kwa Sisi enthusiastic wa Magari
 
Manual ni kwa enthusiast tu mkuu.
 
Upo sahihi kabisaaa...kuna watu huwaambii kitu juu ya manual transmission kwasabb ya Ile ladha ya kubadilisha gear unavyotaka, ndiyo maana serikalini Magari Yao asilimia kubwa ni manual
Kweli mkuu,yale magari ni ya kazi kazi hakuna kuremba.

Hio gearbox (Dsg) niliikuta garage kwny golf gti ikiwa imezingua,ni expensive sana kuinunua
 
Kweli mkuu,yale magari ni ya kazi kazi hakuna kuremba.

Hio gearbox (Dsg) niliikuta garage kwny golf gti ikiwa imezingua,ni expensive sana kuinunua
DSG inakufa clutch tu au shida kwenye control yake ikiwa hiyo DSG ni wet. Dry huwa zinakufa clutch tu mara nyingi.

Vitu vingine vyote 8 ni kama gearbox ya manual. Siyo gearbox ngumu sana kuielewa. Na hata ikifunguliwa ndani inaeleweka na inafanana na manual ila tu inakuwa na shaft nyingi.
 
Safi sana kwa maelezo murua mkuu.
 
Wewe unamshauri mwenzako akae mbali na CVT wakati Dunia ndio inaelekea huko?
Dunia inaelekea Electric mkuu, hizi ni finali tu. Vilevile inavyosemekana kuwa CVT ndiyo future haimaanishi kuwa ni kwa gari zote, CVT itapatikana sana kwenye magari ya budget, PDK, Tiptronic, etc bado zitashamiri sana kwenye performance cars. CVT bado ni technology changa hivyo ni vyema kukaa nayo mbali maana bado kama ipo kwenye majaribio bila kusahau kiwa mafundi wengi hawazielewi hizo transmissions, ndiyo maaana ikiwa na tatizo kidogo tu, fundi atashauri ununue gearbox mpya kwa maaana hajui pa kuanzia. Mimi binafsi gari ya CVT ni never, DCT is the best Transmission ever iwe ni Porsche PDK, Audi S-Tronic, Tiptronic,.. Ni Transmissions zinazofurahisha sana, CVT inaboa mkuu, ila ni nzuri owa watu ambao umri umeenda sana, wakina mama, na woote wasiojali kuhusu performance figures za gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…