Naomba ufafanuzi kuhusu gari aina ya Subaru Legacy

chukua tu Subaru Forester
 
Kuna jamaa yangu analo naonaga linasomaga 6-7 km/l likichanganya speed linafika 8km/l.

Difference lazma ui feel mwamba yani toka 16km/L mpaka 8Km/L safari za sheli za hapa na pale lazima.
Nilichobaini watu wengi hatuyajui hays Magari sema tunajadili. Ni kweli consumption ya subaru legacy kwenye dashboard huwa inasoma kuanzia 5.5 hadi 13 au zaidi. Lakn hiz Namba hazina maana kuwa ikisoma 5.5 ndo Inatembea lita Moja kwa kilometres 5. Hiz gar consumption yako imewekewa kwa 100km. Kwahyo gari yako ikiwa inasoma 6.5 huwa ni kwa 100km yaan maana yake ni 6.5/100km ikiwa na maana kuwa kupata unatembea km ngap kwa lita unachkua 100km/6.5. Mim nina subaru legacy ya 2013 nikiweka full tank inaniambia nitatembea km 748 na nikiwa high way km zinaongezeka, consumption yake inaenda 5.8 na mjini ndo inaenda hadi 12 ikiwa na maana kuwa natumia lita Moja kwa kilometer 8.3

Na uzuri wa hizi gar zina gauge ya utumizi wa Mafuta unapoendesha inakuonyesha kabisa sasa hiv matumizi yako low au uko juu au uko average.

Kuhusu uimara hiz gar ni imaraga sana toka ninunue kitu kikubwa ambacho niliwah kubadili tena ni kwa sabab ya fund aliniingiza cha kike ni sterling lack ambayo nilinunua laki sita na nusu. Fund alikuwa anabdilisha shock up akaongona had sterling racks.

Kuhusu kukimbia ni gar inayo kimbia sana maana yangu inaspeed 240, natural Aspirated engine (engine kavu), CC 1900, na ina uzito wa tani 2.5. May be kwa kuwa yangu nilinunua za soko la Europe ndo maana inaonekana ina unafuu sjuh ila sjuh wengne wanazozimiliki. Shida kubwa tu nayoiona iko chini kwa mbele kiasi kwamba kila napo mwazima mtu lazma bumper ya mbele ipate dosar kidogo.

Kuhusu service ni sawa na gari nyingne tu oil natumia castrol 5W300 laki Moja au lak na kumi na natembea km 10,000. Kikubwa kwenye service haitaki janja janja
 
Hongera sana mtu wangu, kwahio ile prado iliokuwa inasoma 16km/l maana yake inatembea kwa 6.6km/l kwa mujibu wako? 🤣
 
Hongera sana mtu wangu, kwahio ile prado iliokuwa inasoma 16km/l maana yake inatembea kwa 6.6km/l kwa mujibu wako? [emoji1787]
Soma tena maelezo yake kwa umakini kidogo...magari mengi kwenye fuel consumption yako rated kwa 100km...
Kama imeandikwa 16km/l, hiyo iko direct
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…