Nataka kuagiza gari toka Japan, baada ya kupita huku na kule nimeamua ku shortlist magari kadhaa, moja wapo ni hii toyota corolla axio ya 2007.
View attachment 1445940
Corrola axio kama inavyoonekana pichani.
Naomba uzoefu kwa mtu anayetumia gari hii kuhusu changamoto zozote anazokutana nazo.
Pia nimeona automatic transmission yake ni super CVTi, vipi maintenance yake ina changamoto zozote? Pia naweza pata mapendekezo gereji za kuaminika kwa Dar kwa ajili ya kubadili hiyo transmission fluid.
Natanguliza shukrani.
TOYOTA AXIO
Gari hii ilitambulishwa katika soko la japani mwaka 2007 , na kufanya kubadilintaswira ya soko la magari huko japani huku ikipendwa zaidi kwa kuwa nà matumizi madogo ya mafuta,gari hiii ni gari ndogo kwa matumizi ya familia na inafaa sana hata kwa watu wanaofikiria biashara za kusafirsha km uber na tax
Baadhi ya vitu ambavyo vipo katika gari hii ni
Umbo ni Saloon
Extras: AC, Double Din Stereo/Navigation, Fog Lights, Heater, Spoiler
Safety Features: ABS, Airbags
Exterior Features: Alloy Rims, Fog Lights, Spoiler
Interior Features: A/C, Double Din
Baadhi ya magari ya TOYOTA AXIO yametengenezwa kwa ajili yabsoko la ndani ya japni tu( JDM ) Lkn yamesafirishwa na kuja kuuzwa katika mazingira ya afrika na jambo la kishangaza ni kuwa gari hiii lina dumu na kuvumilia miundo mbinu ya afrika kuzidi hata CARINA T.I
Upande wa injini
Toyota Axio inakuja na machaguo mawili 2 engine sizes: 1500cc na 1800cc huku yakiwa na utofauti mkubwa sana ... . Kwa injini ya 1.5L inakuja na machaguo mawili grades; 1Toyota Axio X na 2 Toyota Axio G. Kwa injini ya 1.8L, inakuja na chaguo moja tu , Toyota Axio Luxel. Toyota Axio Luxel inakuja na sifa nyingi zaidi kuliko ,Axio X kama rear spoiler, alloy wheels, navigation, na fog lights.
GRADE ZA GARI HI
[emoji3541]1.5 Litre / FF/ Automatic or Manual / 1NZ-FE Engine / DBA-NZE 141G
[emoji673]1.5 Litre / 4WD/ Automatic / 1NZ-FE Engine / DBA-NZE 144G
[emoji3541]1.8 Litre / FF/ Automatic / 2ZR-FE Engine/ DBA-ZRE 142G
[emoji673]1.8 Litre / 4WD/ Automatic / 2ZR-FE Engine/ DBA-ZRE 144G
[emoji3541][emoji3541]*FF stands for Front Drive, Front Engine
Upande wa mafuta hii ni gari bora sana katika kipengele hiki kwani inaishinda hata CARINA T.I yaani inafaaa sana hebu tuangalie
[emoji3541][emoji3541]Toyota Axio 1500cc inatumia km 18.2 kwa lita 1
[emoji3541][emoji3541]Toyota Axio 1800cc inagumia km 15 kwà. lita 1
Kama sio mtu wa safari za masafa marefu nakushauri nunua yenye cc1500 upate raha duniani
[emoji91][emoji91][emoji91]TANK LAKE LINACHUKUA LITA 60
Upande wa GROUND CLEARENCE
kwa kuwa gari hii ni saloon lakina bado wamejitahidi sana kuipa uvungu mkubw wa chini ina 6.3 inch ,na inafaa kwa matumizi yote vijijin na mjini yaani popote pale unaendesha gari hii bila hofu
Changamoto za gari hii
Kwa kuwa injini ya Toyota Axio is1NZ-FE(1.5L) imetumika katika magari ya toyota tangu mwaka T 1999. Ni injink nzuri ambayo inaweza kwenda mwendo mrefu na kuvumilia sana pasipokuwa na matatizo yoyote . Baadhi ya changamoto zilizozoeleka ni
1. Excessive oil consumption
2. Engine Vibrations
3. Engine Knock
Kwa injini ya chaguo la pili 2ZR-FE (1.8L) ambayo imeanza kutumika tangu 2007. Kama ilivyo 1NZ, injini hii isipotunzwa vizuri huwa na matatizo yafuatayo
1. Excessive oil consumption
2. Irregular idling
3. Engine Knock
Ninachopenda katika gari hii
[emoji91]Matumizi ya mafuta
[emoji91]Spare za kumwaga mpk uchochoroni
[emoji91]Bei ya gari ni rahic
[emoji91]Boot kubwa
[emoji91]Barabara yoyote linapita
Mwisho niseme
Kama unafikiria kununua gari ndogo kwa ajili ya biashara zako basi haujakosea chaguo sahihi ni AXIO , ni gari imara sana haiharibiki hovyo
Na kwa ndani ina viti vizuri kbs
Mkuu kwa hayo machache nadhani yatakufaa
sent from HUAWEI