Naomba ufafanuzi kuhusu michango yangu ya PPF

Je, wakati wa unastaafu .Pension wanakulipaje sasa.Utakuwa unachukua kote kuwili. PPF umechangia 10years na labda NSSF 7 years inakuwaje
Itachanganywa ili mtu apate mafao mazuri, nimeulizia nikaambiwa hivyo. Wakati wa kustaafu wataangalia kule ambako umemalizia ndiyo wstahamushia huko.
 
Ndiyo maana nakuambia wataiunganisha michango yako from both ili uwe umequlify kulipwa pensheni
 
Kwa mujibu wa sheria mpya iliyounda hii mifuko 2, NSSF kwa private sector na PSSSF kwa walioko serikalini ni kwamba kuna utaratibu wa kuunganisha michango ili mchangiaji wakati wa kuchukua mafao achukue kwa pamoja na aweze kunufaika zaidi.
Mpaka sasa hakuna michango iliyounganishwa.
 
Michango yako iliyoko PSSSF itabaki huko huko na wakati wa kuichukua utafuata taratibu za huko huko PSSSF kuipata.

Hivyo hivyo huku NSSF pia utafuata taratibu zao kupata haki zako. Hakuna muingiliano wowote wala kuunganishana.
Hili Ni tatizo Sasa.

Sababu michango yako ikifikia miezi 180 (miaka 15) unakua qualified kupata monthly pensions apart from Gratuity.

Sasa Kama NSSF iko miezi 100 na PSSSF iko miezi 80 si utajikuta inanyimwa kote kote?
 
PSSSF kazi iendelee,wastaafu waendelee kuteseka mtaani.
 
Mkuu @NALO LITAPITA
kwema, Nilikuwa na swali kama hili. Je kwako ulifikia wapi baada ya kufuatilia ukiunganisha na maelezo ya wadau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…