Naomba ufafanuzi kuhusu railway levy

Naomba ufafanuzi kuhusu railway levy

Nyumisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2010
Posts
13,499
Reaction score
19,292
Salaam wana JF,

Kama heading inavyojieleza kuna kiasi cha pesa kinachokatwa kwenye kila gari inayoingizwa nchini kupitia bandarini, labda na kwingineko kinaitwa railway levy.

Mimi kwa uelewa wangu nadhani hii pesa ni kwa ajili ya maendeleo ya reli hasa ujenzi na ukarabati. Katika ufahamu wangu wa ujenzi wa reli ya SGR tangu kipindi cha mwendazake kuna pesa nyingi zimeshakopwa kugharimia huo mradi wa SGR ingawaje tuliambiwa kwamba zingetumika pesa za ndani.

Je, tangu pesa za railway levy zianze kukusanywa hazijatosha kugharamia mradi wa SGR angalau kwa asilimia 70 hadi tuanze kukopa? na kwa namna hali inavyoenda huo mradi unaweza kuchukua miaka mingi kukamilika kutokana na kuhitaji pesa nyingi.

Naomba wajuvi waje watiririke uelewa wao kuhusu jambo hili.
 
Me naona ni kuongezeana tozo zisizo na maana.
 
Hata magufuli angeachwa kwa miaka 20 ijayo sgr isingekamilika na nchi hii ingetumbukia kwenye madeni ya ajabu.
 
Hata magufuli angeachwa kwa miaka 20 ijayo sgr isingekamilika na nchi hii ingetumbukia kwenye madeni ya ajabu.
Ndio maana Mungu aliamua kumtanguliza mapumzikoni,kusudi Watanzania tupate maendeleo ya kweli
 
Back
Top Bottom