Kwa kuwa unajua kuhusu usajili, twende kwenye namna ya kufanya kazi.
Kesi ya madai inapokwisha kunakuwa na mshindi na mshindwa, sasa kama kuna jambo mshindwa ameamriwa na mahakama kulitekeleza na asilitekeleze, mshindi wa kesi anaenda tena mahakamani kuomba kati ya mengine, nguvu itumike ili jambo hilo litekelezwe, kwa kuwa mahakama haifanyi kazi za nguvu hapo ndipo madalali wa mahakama sasa wanapoingia, unateuliwa ukatekeleze hiyo amri, mfano kubomoa nyumba au kuuza mali ya mshindwa nk. Gharama ya kufanya kazi yako zimeelekezwa kwenye sheria ya minada na mara nyingi ni makubaliano kati yako na mteja wako.
Kwa kuwa mshindwa aligoma kutekeleza amri usifikiri atakubali kirahisi amri hiyo kutekelezwa na mtu mwingine, hivyo lazima nguvu itumike, dalali uwe na mabaunsa wa kufanya kazi hiyo, upate ulinzi wa polisi nk
Sambamba na hilo la kufanya utekelezaji wa amri za mahakama, pia madalali hutumika kusambaza nyaraka za kesi (za mahakama) kwa pande za kesi. Nyaraka kama samansi, hati za madai nk. Si unajua mkiwa na kesi mara nyingi mnakuwa maadui!! Ili mdai asijepigwa risasi na mdaiwa anapopeleka samansi kwa mdaiwa basi hapa ndipo madalali wanatumika, sababu wao wanakuwa wapo kazini na hawahusiani chochote na ugomvi au madai ya mdai na mdaiwa. Gharama ya kupeleka wito ndani ya mji ni shilingi elfu 10 hivi.
Pia soma hapa
https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=announcements/pdf&id=66 Tangazo limeeleza kila kitu