Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 16,879
- 31,253
Mchango wa Mwenge sio lazima ni ihari kwa watu wote,hakuna anayekulazimisha acha upotoshaji.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]Hoja za mkuu Mpwayungu Village zina mashiko kuhusu uelewa na uwezo wa waalimu
Kuna mida yupo sahihiHoja za mkuu Mpwayungu Village zina mashiko kuhusu uelewa na uwezo wa waalimu
Ha ha ha leo hii mshikeshike huu upo ndani ya kijiji cha ikuti wilaya ya Rungwe😂😂😂😂kumbe hii inatokea sehemu nyingi.😳😳kule vijijini ndio wajasiriamali wanalazimishwa kindakindaki wakafanyie biashara zao uko kwenye mwenge, kuanzia mama ntilie, Bar adi pombe za kienyeji, ukikamatwa haujaenda kwenye mwenge na bidhaa zako unadakwa unalipa elfhamsini eroo
Wewe ungelichanga ama kuahidi ili kuua soo.Wakuu, sina haja ya kuwasalimia kutokana na mvurugo bila kusahau matusi ya Mkuu Mpwayungu naomba kuuliza wajuvi hivi mwalimu akishindwa kuchangia mchango wa MWENGE ambao ni shilingi elfu tano katika halmashauri hii anakuwa amemkosea nani kwa sababu naona ni wazi tunatafutana lawama. Kuna wananchi wengi tu lakini hawabanwi, why Walimu?
Mikwara miiingi mara majina sijui yanatumwa kwa mkuu wa wilaya kwa wasio changia mwenge kwa Nini mnatulazimisha kama ni lazima si muwe mnakata hukohuko kabla mshahara haujatoka?
Binafsi sioni mantinki naona ni uonevu wa Hali ya juu mwalimu amekua ndio jalala la majanga huo mwenge wenyewe ukifika mwalimu hatambuliwi watu wanatafuna vyuku kwa michango ya walimu masikini Serikali tafadhali msituonee hivi kuweni na chembe ya huruma magoli mnanunua milioni20 mchango wa MWENGE unawashindaje?
Mwenge na uheshimiwe ni tunu ya TaifaWewe ungelichanga ama kuahidi ili kuua soo.
Mimi ninavyojua wewe umebanwa na afisa elimu ambaye naye kabanwa na mkuu wa idara.
Mwenge unapokaribia Wilaya husika, basi huitishwa kikao kwa Dc akishirikiswa na Mkurugenzi na wakuu wake wa idara kujadili michango ya "mafuta" ya mwenge.
Wanakamati hao hutozana hela kubwa kubwa kwa lazima na kisha kupeana majukumu ya kuchangisha staff walio chini ya idara zao, kabla Mwenge haujafika.
Wewe kama ni mwalimu mshika chaki waweza kataa kisiasa kwa visingizio chochote na mwenge ukushapita unapita na kadhia zake.
Lakini kwa safu iliyopo Wilayani,(KUU pamoja na mkurugenzi) mchango huo huwaga ni wa lazima na wala si wa kubembelezana.
Aliyekutuma uwe mwalimu ni Nani!?Wakuu, sina haja ya kuwasalimia kutokana na mvurugo bila kusahau matusi ya Mkuu Mpwayungu naomba kuuliza wajuvi hivi mwalimu akishindwa kuchangia mchango wa MWENGE ambao ni shilingi elfu tano katika halmashauri hii anakuwa amemkosea nani kwa sababu naona ni wazi tunatafutana lawama. Kuna wananchi wengi tu lakini hawabanwi, why Walimu?
Mikwara miiingi mara majina sijui yanatumwa kwa mkuu wa wilaya kwa wasio changia mwenge kwa Nini mnatulazimisha kama ni lazima si muwe mnakata hukohuko kabla mshahara haujatoka?
Binafsi sioni mantinki naona ni uonevu wa Hali ya juu mwalimu amekua ndio jalala la majanga huo mwenge wenyewe ukifika mwalimu hatambuliwi watu wanatafuna vyuku kwa michango ya walimu masikini Serikali tafadhali msituonee hivi kuweni na chembe ya huruma magoli mnanunua milioni20 mchango wa MWENGE unawashindaje?