Naomba ufafanuzi kuhusu ulazima wa mwalimu kulipia mchango wa Mwenge

Kumbe kuna watu wanachangia mwenge😳😳😳
Sijawahi changia huo upuuzi.
 
kule vijijini ndio wajasiriamali wanalazimishwa kindakindaki wakafanyie biashara zao uko kwenye mwenge, kuanzia mama ntilie, Bar adi pombe za kienyeji, ukikamatwa haujaenda kwenye mwenge na bidhaa zako unadakwa unalipa elfhamsini eroo
 
Ili tusikumbane na mambo kama haya vema tukubaliene na Serikali katika ubinafsishaji inawezafikia hatua wanaweza kuubinafsisha huu mwenge
 
kule vijijini ndio wajasiriamali wanalazimishwa kindakindaki wakafanyie biashara zao uko kwenye mwenge, kuanzia mama ntilie, Bar adi pombe za kienyeji, ukikamatwa haujaenda kwenye mwenge na bidhaa zako unadakwa unalipa elfhamsini eroo
Ha ha ha leo hii mshikeshike huu upo ndani ya kijiji cha ikuti wilaya ya Rungwe😂😂😂😂kumbe hii inatokea sehemu nyingi.😳😳
 
Wewe ungelichanga ama kuahidi ili kuua soo.

Mimi ninavyojua wewe umebanwa na afisa elimu ambaye naye kabanwa na mkuu wa idara.

Mwenge unapokaribia Wilaya husika, basi huitishwa kikao kwa Dc akishirikiswa na Mkurugenzi na wakuu wake wa idara kujadili michango ya "mafuta" ya mwenge.

Wanakamati hao hutozana hela kubwa kubwa kwa lazima na kisha kupeana majukumu ya kuchangisha staff walio chini ya idara zao, kabla Mwenge haujafika.

Wewe kama ni mwalimu mshika chaki waweza kataa kisiasa kwa visingizio chochote na mwenge ukushapita unapita na kadhia zake.

Lakini kwa safu iliyopo Wilayani,(KUU pamoja na mkurugenzi) mchango huo huwaga ni wa lazima na wala si wa kubembelezana.
 
Mwenge na uheshimiwe ni tunu ya Taifa
 
Aliyekutuma uwe mwalimu ni Nani!?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Poleni sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…