Naomba ufafanuzi kuhusu usajili wa plate number za magari

Naomba ufafanuzi kuhusu usajili wa plate number za magari

Master C mimd

Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
46
Reaction score
55
Wakuu naomba kufahamu kitu kimoja kwa anaye jua, hiviusajili wa hizi plate number ukoje?

Mfano unaweza nunua gari ukaifanyia usajili safi kabisa ukapewa mfano DPT then ukiingia barabarani unakuta plate number zinasoma DST huko, hili swala limekaeje?
 
Maana yake baada ya usajili wa gari. Haikuwa Mwisho Wa Usajili Wa Gari Tanzania, Yaani Usajili Unaendelea Kila Iitwapo Leo
 
Watanzania ni malimbukeni sana ya Number, Imefikia mtu mwenye namba A, anaonekana kapitwa na wakati, ndo wale anakukuta anakuambia "mbona umezeeka ivi" Ivi kweli hamjaonana miaka 15, afu uwe vile vile! utakua mzima kweli! Si inabidi ulazwe hospitali.

Tuje kwenye mada, hizo namba mnazojivunia ni mpya leo, baada ya miaka 3 zitakua za zamani, je utatupa hilo gari?
 
Watanzania ni malimbukeni sana ya Number, Imefikia mtu mwenye namba A, anaonekana kapitwa na wakati, ndo wale anakukuta anakuambia "mbona umezeeka ivi"
Ivi kweli hamjaonana miaka 15, afu uwe vile vile! utakua mzima kweli! Si inabidi ulazwe hospitali.

Tuje kwenye mada, hizo namba mnazojivunia ni mpya leo, baada ya miaka 3 zitakua za zamani, je utatupa hilo gari?

Mkuu mimi siko huko, kitu nilichotak kujua ni kimoja tu labda unashidwa nielewa,mfano wewe umetoka kusajili gari yako leo ukapewa DSR then unaingia barabarani unakutan na DTP huo ni mfano tu, ndio nikaona niulize labda kuna kitu mimi sikijui
 
Mkuu hiyo kasi unayosema ya DSR mpaka DTP inaweza isiwepo ila kutokea DSA kwenda DSL ni kazi rahisi sana. Nadhani inatokana pia na mtindo wa wazoefu kuhold usajili mpaka Herufi mpya kuja. mfano kiTZ kuna utofauti mkubwa sana wa DSZ na DTA kwa hiyo namba zina mtindo wa kukimbia mwanzoni alafu kutambaa mwishoni kwenye herufi karibu na Z.

Pia meli zinashusha magari mengi na zinaweza kufululiza, ikitokea hiyo Herufi zinaweza kupaa, sasa kama gari lako liliwahi kusajiliwa ila likachelewa kutoka au kuchukuliwa kwa wakala. Baadae likakutana na gari ambalo limechelewa kusajiliwa ila limewahi kuchukuliwa, hapo hiyo jump inaweza kutokea
 
Wengi nahisi hamjamuelewa mleta mada.

Mleta mada kuna swala labda hulielewi, umesajili TRA au umetoka kununua yard?

Nimeuliza kwa sababu kuna wenye yard husajili kabisa gari na mteja unakuja chukua na kuondoka.

Yawezekana ulikutana na case hiyo. Hivyo ukatoka na DSR na mtaani unakuta DTH

Pili

Kuanzia July baada ya bajeti mpya mtu utaweza sajili gari kwa number yoyote as long as haijasajiliwa, kwa pesa sh. Laki tano.

Hivyo kuanzia julai usishangae kukutana na gari number T XXX ZPB mfano.
 
Wakuu naomba kufahamu kitu kimoja kwa anaye jua, hiviusajili wa hizi plate number ukoje?

Mfano unaweza nunua gari ukaifanyia usajili safi kabisa ukapewa mfano DPT then ukiingia barabarani unakuta plate number zinasoma DST huko, hili swala limekaeje?
Hiyo Gari Kama umeisajili TRA (Bandarini) hakuna kitu Kama hicho. Ila Kama umenunua Showroom inawezekana kabisa.
 
Hiyo Gari Kama umeisajili TRA (Bandarini) hakuna kitu Kama hicho. Ila Kama umenunua Showroom inawezekana kabisa.
mkuu unaweza kutufafanulia kwenye hilo kwanini bandarini isiwezekane na showroom iwezekane?
 
mkuu unaweza kutufafanulia kwenye hilo kwanini bandarini isiwezekane na showroom iwezekane?
Bandarini ndio kwanza gari imeingia, so watakupa number ambayo ni "Current" at that particular time.

Showroom (ambayo sio bonded warehouse) ni mtu aliyanunua kipindi kilichopita akayasajili kwa number za kipindi hicho sasa anayauza.
 
Mkuu hiyo kasi unayosema ya DSR mpaka DTP inaweza isiwepo ila kutokea DSA kwenda DSL ni kazi rahisi sana. Nadhani inatokana pia na mtindo wa wazoefu kuhold usajili mpaka Herufi mpya kuja. mfano kiTZ kuna utofauti mkubwa sana wa DSZ na DTA kwa hiyo namba zina mtindo wa kukimbia mwanzoni alafu kutambaa mwishoni kwenye herufi karibu na Z...

Shukrani mkuu, umenijibu na nimeelewa kitu
 
Jamaa haelewi kaingia kitaa na gari mpya ghafla ishakuwa ya zamani [emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app

Ha ha niliumiza sana kichwa kwa lengo la kutaka kujua tu, maan niliikuta gari showroom nikalipia tukaifanyia usajili ila kuingia nayo kitaa nakuta plate number zimepaa kinoma sasa ikawa waswasi wangu isije kuwa niliuziwa gari iliyotumika, hiyo ndio sababu ya kuandika huu uzi
 
Huyo wa Showroom ye alinunua akaisajili kitambo tu. Sasa unazokutana nazo Ni zile zilizosajiliwa baada ya hii ya showroom, Hiyo pekee ndo sababu.
 
Pili

Kuanzia July baada ya bajeti mpya mtu utaweza sajili gari kwa number yoyote as long as haijasajiliwa, kwa pesa sh. Laki tano.

Hivyo kuanzia julai usishangae kukutana na gari number T XXX ZPB mfano.
Huu mtindo wataufanya kwa mwaka mmoja tu halafu watauondoa. Wizi wa magari na namba feki zitatapakaa. Sasa hivi hatuna gari zenye mamba inayoanza na E, na hivyo gari ikionekana na namba inayoanza na E, hata raia wa kawaida tu lazima ajue kuwa ni feki.

Baada ya hapo, wenye kujua kuwa namba ni feki watakuwa ni Police Traffic na TRA pekee, raia wengine hatajua!
 
NewGapi,
Hivi walivyosema kusajili kwa 500,000 wanamaanisha nini? Maana mfano umenunua gari Japan ukalipa makorokoro yote hadi ile registration ya 500,000 ina maana utatakiwa ulipie tena 500,000 ili upate T XXX JPM?
 
Back
Top Bottom