HOJA Naomba ufafanuzi kuhusu vigezo vya udahili wa kozi ya Doctor of Medicine (MD)

HOJA Naomba ufafanuzi kuhusu vigezo vya udahili wa kozi ya Doctor of Medicine (MD)

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Naomba ufafanuzi kuhusu vigezo vya udahili wa kozi ya Doctor of Medicine (MD).

Mwongozo wa TCU unaeleza kuwa mwombaji anatakiwa awe alisoma somo la Physics katika ngazi ya O-Level. Je, wanafunzi waliosoma katika shule za ufundi (Technical Secondary Schools), wakasoma mchepuo wa Science Engineering na baadaye kuchaguliwa kusoma PCB katika A-Level, hawastahili kujiunga na kozi ya Doctor of Medicine?

Ikiwa walikidhi vigezo vya kuchaguliwa kusoma PCB A-Level, kwa nini wanapoomba kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wanaonekana kutostahili? Tunaomba TCU na mamlaka husika kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili ili kuondoa mkanganyiko kwa waombaji.
 
Ninavyojua mimi kwa uzoefu wangu Mdongo Engeneering Science mara nyingi inakuwa mbadala kwa wale ambao hawakusoma Physics

UNgeeambatanisha na TCU GuideBook kwanza hapa Mkuu
 
Waliosoma shule za Tech, kisha Advanced Level wakasoma PCB wanaruhusiwa kusoma kozi za Afya.

Nina mdogo wangu yuko mwaka wa 3 chuo na alisoma kwa mtiririko huo.
 
Wakati mwingine muwe mnaomba vyuo nchi za nje kupitia scholarships, Dunia imekua Kijiji achaneni na mambo ya ujima!
Kozi zingine sawa, ila afya kama hujakidhi vigezo vya humu ndani, kukimbilia nje wasithubutu, watakuja kulia na degree yako ya nje mkononi. Shida kubwa sana ipo kwenye mabaraza yanayosimamia izo taaluma za afya
 
Wakati mwingine muwe mnaomba vyuo nchi za nje kupitia scholarships, Dunia imekua Kijiji achaneni na mambo ya ujima!
Unawajua TCU kwanza na Mabaraza ya Kitaaluma siku ukirudi Utafute leseni

Nina Mwanangu ana PCM akasoma India BPharm kurudi Bongo intern tu kasota vibaya mnoo hadi akaamua kufanya kazi zingine tu
 
UDOM huwa wanazingua wanaosoma engineering science,ila MUHAS hawana hiyo cha msingi ufaulu wa advance among 200 bora.
.
 
Hii nchi ukisema ni SHITHOLE kuna wanaopinga.

Yaani hakuna logic ya kuwabania watu kusoma wakati wanauwezo.Mtu kasoma na kafaulu unamnyima leseni ya kufanya kazi.Ukianglia hao wafamasia wanaonyima wenzao fursa hawajawahi hata kutengeneza kidonge cha muarobaini,,,shwaini kabisa!!!

Uafrika especially utanzania ni laana.
Hili baraza famasi nafikiri ndio linaongoza kwa fujo na vita na wanafunzi😀
 
Back
Top Bottom