Naomba ufafanuzi taasisi ya elimu (Chuo) kutoa gawio kwa Serikali

hivi NIDA wanafanya biashara gani ya kuwaingizia faida hadi watoe gawio?
 
Hahaa awamu ya comedy
 
FUTUHIIIII NDIO NI FUTUHI.

Wanajua wanahaibika kwenye UCHAFUZI ndio maana wanaleta taarifa ya Styne kuzuia ndege maa kuhamia ikulu mara magawio ili mradi kuficha AIBU ya UCHAFUZI hahahahahahaahaaaaaa.
 
Sasa vyuo vikuu karibu vyote vinaongozwa Kwa hasara/deficit ,na vinategemea ruzuku,gawio linatoka kwenye fedha zipi?
 
Tanzania ina vichekesho sana sasa NIDA anatoa gawio kutoka katika faida gani aliyopata?
 
Hakuna taasisi isiyo na changamoto. Ww unadhani TPA hawana shida na upanuzi wa bandari, au unafikir hawana madeni
Kiongozi, TPA ni sawa na ndiyo maana sijawataja. Hao wanafanya biashara.
IFM na taasisi nyingine za elimu ni simply huduma kwa jamii.
Kesho mtasikia hospital zinatoa gawio!
 
Kama wanafanya biashara kwann wasitoe??? Changamoto za ndani hazizuii kutoa gawio.. na pia gawio linapatikana baada ya kutoa matumizi yote ( Expenditures) fedha inayobaki ndo serikali inapokea, na ninyi mnaanza shughuli za mwaka mwengine wa fedha
Kiongozi, TPA ni sawa na ndiyo maana sijawataja. Hao wanafanya biashara.
IFM na taasisi nyingine za elimu ni simply huduma kwa jamii.
Kesho mtasikia hospital zinatoa gawio!
 
Kama wanafanya biashara kwann wasitoe??? Changamoto za ndani hazizuii kutoa gawio.. na pia gawio linapatikana baada ya kutoa matumizi yote ( Expenditures) fedha inayobaki ndo serikali inapokea, na ninyi mnaanza shughuli za mwaka mwengine wa fedha
Naelewa vyema jinsi taasisi za elimu zinavyoendeshwa na matatizo yake. Ni sawa na kuazima jamvi msibani.
 
Hyo ada unataka iende wapi jiulize private school wanapataje faida si ada hzo simpo
 
IFM ni chuo cha serikali ambapo mishahara yote ya watumishi inalipwa na serikali ila inakusanya ada kwa wanafunzi.
Idadi ya wanafunzi kuanzia certificate hadi ngazi ya masters hawapungui 5000.
Kila mwanafunzi akitoa ada ya milioni moja tu kwa mwaka nje ya hostel ni hela nyingi sana. toa matumizi ya maji, umeme, mafuta ya gari kiasi kinachobaki ndio hilo gawio
 
Ni aibu kwa taasisi za elimu kugeuka kuwa vitega uchumi. Ni ndani ya vyuo hivi wanafunzi wanashinda au kulala njaa , na wengi kukosa hela ya ada, wengine kugeuka vibaka, machinga, bodaboda na changudoa ili kujikimu. Kumbe gharama zinapandishwa kupata gawio.
 
Naelewa vyema jinsi taasisi za elimu zinavyoendeshwa na matatizo yake. Ni sawa na kuazima jamvi msibani.

Wewe huelewi chochote, au unadhani Serikali inaendeshwa mithili ya familia yako? Matengenezo yote unayoyaongelea katika Taasisi za umma yana bajeti yake, Mtu hawezi kukurupuka tu na kutumia fedha kwa tatizo ambalo hazikuelekezwa kwake. Muda mwingine tuwe tunatumia akili kidogo tu kufikiri, maana inawezekana nyie ndo future leaders wa nchi hii, lakini msipojielimisha mambo haya madogo mnakuwa janga la Taifa.
 
Sasa hiyo ni biashara au.. Ndo utasikia jeshi nalo limerudisha gawio au polisi.. Hizo ni gharama tu za uendeshaji sasa mbona vitambulisho havitolewi
Ukipoteza Kitambulisho Unalipa Tshs 20000/=
Uweze Kupatiwa Kingine, Wanastahiri Kulipa Gawio Serikali
 
Tatizo la humu kila mtu mjuaji kutoa gawio ni muhimu hata kama ni milioni 10 tu. Taasisi zijalibu kupunguza warsha na makongamano yasiyo na tija au kujinunulia magari ya kifahari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…