Naomba ufafanuzi toka wafuasi wa CCM na viongozi wao - Mabeberu ni kina nani, ni nchi wahisani au wafadhiri?

Maana:

1. Ubeberu ni ubepari uliokomaa
2. Beberu-Ni mbuzi dume.
 
Majina hutofautiana kulingana na kile unachofanya.

Ukiwa unalima unaitwa mkulima.

Unafundisha unaitwa mwalimu.

Ukitunyonya wewe ni beberu.

Ukitupea msaada unakuwa mfadhili au mhisani

And the like.
 
Kama ccm huwa wanatumia neno mabeberu kumaanisha wale wanaoinyonya nchi yetu basi itoshe kusema
Ccm inaongoza kwa kuwa na mabeberu wengi wanaoinyonya nchi yetu tena kwa mabavu na kwa sheria za kinyonyaji.
UKishaamua kwamba kwa ujumla nchi fulani ni bebebru anatunyonya, utamsifiaje kuwa mfadhiri na mhisani kwa upande mwingine? Na hivi nchi inawezwa kulazimishwa kunyonywa? Kama tunaona wanatunyonya basi tukate uhusiano nao kabisa!
 
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
Hao magu anaowaita mabeberu ndio anamtuma Kabudi kila siku kwenda kuwaomba fedha na kusamehewa madeni.
 
Hao Wanaowaita wazungu mabeberu ndio wanyonyaji wakubwa wa watanzania kuwazidi hata hao wazungu.
 
Hahaha juzi walipokea hati za utambulisho wa beberu kuu.
 
Hao magu anaowaita mabeberu ndio anamtuma Kabudi kila siku kwenda kuwaomba fedha na kusamehewa madeni.
Kwa kweli ni kukosa busara na hekima ya uongozi. Unajua Magufuli anataka kujifanya Nyerere kwa kuleta lugha hii karne hii. Hii lugha ilikuwa ya enzi zile za Nyerere, haifit katika ulimwengu wa leo. Na zaidi Nyerere alijua sana wapi panafaa kutumia hili neno, siyo kama rejareja za Magufuli au CCM - wanalitumia kama neno la jumla kumaanisha mataifa ya nje. Eti Chadema nendeni kwa marafiki zenu mabeberu - walewale ambao CCM inawaita wafadhiri!
 
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
Mabeberu ni wale waliokopesha awamu ya tano matrilioni kujenga miradi ya hovyohovyo
 
Nilitarajia watu wa Lumumba kunisaidia kwa hili haraka, kama wanavyojitokeza haraka kwenye thread nyingine ukitaja neno CCM. Vipi, hii imekuwa ngumu kumeza?
tangu mwalimu JKN atutoke (RIP mzee wetu), tumepoteza mwelekeo wa hata tunachokipigania kwenye chama chetu.

yule mbunge "Bwege" hakukosea kabisa.... tunatoa jibu linalofanana kwa maswali 2 tofauti na yanayokinzana.

tunaangaliaga upepo unakovumia na sisi ndiyo huko huko tunakwenda.
 
binafsi naona viongozi wetu hawatutendei haki hasa pale unapokuta wananchi hawana uhuru na vyombo vya habari pia bunge kufungwa na kutorushwa wanatunyima haki zetu za msingi kujua yanayoendelea ni kama tumefungiwa chumbani vile
 
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
Mabeberu ni wazungu au watu wowote wanaotukosoa, lakini watu hao hao wakitupongeza ( low middle income country kwa mfano) hao siyo mabeberu. Ila wakitusoa kwa mfano wakisema hatufuati democrasia hapo wanaitwa mabeberu, wakitupongeza kwamba tumejenga daraja na kupambana na ufisadi kibao kinageuzwa, hapo siyo mabeberu ni wahisani.
 
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?

Tanzania na wanasiasa wake hii ni utamaduni wao. Kila siku kuziita nchi za nje kama wakoloni, mababeru, masultani na adui wa nchi, lakini wakati huo huo wanawakimbilia na kuwapigia magoti kila leo kuomba misaada kwao na kuwaita marafiki wa nchi hii.
 
Hivi karibuni hili neno limekuwa likitumika kila wakati, na kuna wakati namsikia hata Raisi Magufuli akilitumia - mabeberu. Nimeona kuwa wakati fulani hata vyama vya upinzani wakiambiwa ni marafiki wa mabeberu.

Wakati fulani nimeona kwamba neno mabeberu linaelekezwa kwa mataifa tajiri ya nje. Lakini ajabu watu walewale wanayoyaita mataifa hayo mabeberu wamekuwa pia wakiyaita nchi wahisani, wafadhiri, marafiki nk.

Hivyo nimejiuliza sana - mabeberu maana yake nchi wahisani au wafadhiri au nchi rafiki kutegemea unaongea na nani?

NImejiuliza pia ikiwa nano mabeberu linatumika tu katika unafiki wa kisiasa, kama vile jirani yako akiwapo unamwita rafiki, lakini pale asipokuwapo unawita mshenzi.

Hivyo badala ya mie kuumiza kichwa kujua hasa mabebebu ni nani, nineomba wale wanaolitumia neno hili, wengi wakiwa wafuasi na viongozi wa CCM, watupe ufafanuzi mabeberu hasa ni kina nani. Je bebeu ndio huyo huyo mfadhiri au mhisani?
Beberu ni mtu yeyote-mweupe :-
1., anayependa utawala wa sheria,

2. haki za binadamu,

3.watu kutotekwa,

4.kesi ziendeshwe kwa uwazi,

5. mashehe wasikae ndani bila kesi ,

6. watu kutopotea,

7.anaywajuza watuhaki zao kama kujua hali zaafya, idadi ya watu na umaskini.
 
Back
Top Bottom