Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja waje wakupe muongozo vizuri ila nachofahamu hii gari ni hybrid kama ilivyo toyota priusMsaada kwa anayefahamu au amewahi miliki hii gari changamoto zake na uzuri wake anisaidie nataka kuiagiza
Hii gari imekaa kama Prius Hybrid from ToyotaMsaada kwa anayefahamu au amewahi miliki hii gari changamoto zake na uzuri wake anisaidie nataka kuiagiza
Msaada kwa anayefahamu au amewahi miliki hii gari changamoto zake na uzuri wake anisaidie nataka kuiagiza
Unaagiza japan mkuuKama ni hybrid hilo betri likifa bongo hapa nalipataje
Honda ni gari nzuri sana. Tatizo kuu ni upatikanaji wa vipuri ni tatizo kubwa sana.Msaada kwa anayefahamu au amewahi miliki hii gari changamoto zake na uzuri wake anisaidie nataka kuiagiza
Umemaliza kila kitu..HONDA INSIGHT
[emoji616]HONDA INSIGHT, hii ni brand moja matata sana umbo lake natokea kulipenda sana ni SUV ,honda hawajawahi kuniangusha hata siku moja wapo makini sana katika uundaji na usanifu wa magari ...wanagari nyingi ni nzuri sana....na imara ndio maana MAREKANI NA ULAYA honda inafanya vizuri kuliko toyota
[emoji106]Body Type:Hatchback
[emoji106]Extras:Reverse Camera
[emoji106]Safety Features:ABS, Curtain Airbags, Front Active [emoji106]Headrests, SRS Airbags, TRC, VSA
[emoji106]Exterior Features:Alloy Rims, Fog Lights
[emoji106]Interior Features😀VD player, USB Charging Port
[emoji616]Honda inight ni gari inayokuja na technolojia ya hybrid na kuifanya utumiaji wake wa mafuta kuwa mdogo sana ....na kulifanya lipendwe kwa matumiz na kuwa rafiki wa mazingira ….kutokana nankutumia mfumo wa umeme na mafuta kidogo gari hili na puric c brand ya toyota kwa sehemu kubwa yanaingiliana sana spear na vitu kadhaa hata umbo usanifu wa kihandisi walishirikiana kutokana na mkataba wa kushirikiana
[emoji616]Linakuja na nafasi ya kukaaa watu 5 kwa ndani huku likiwa na nafasi kubwa nzuri kwa kweli honda nawapa heko [emoji106] maana wanajua sana boot ya
kutosha , na hivyo kulifanya lifanye vizuri sokoni na kuishinda TOYOTA PURIC C katika mauzo na kukubalika halafuu bei ikiwa ya kwaida sana
[emoji616]Kwa ufupi tu honda insight mpk sasa imepitia vizazi vitatu vya uundaji
[emoji3533]1st ilijulikana kama ZE1 Abayo ilizalishwa tangu mwaka 1999-2006
[emoji3533]2nd ilijulikana kama ZE2 Ambayo ilizalishwa tangu mwaka 2009-2014
[emoji616]3rd ilijulikana kama ZE3 2014 hadi leo
Upande wa injini sasa hawa bwana hawajawahi kabisa kufanya kosa kama walivyo air bus katika kuunda ndege , na honda ndio wapo next levol wanakuja na injini yenye cc za kimaskini amabayo inamfaa mtu hata bila kutoka jasho
[emoji123]Honda isightbinakuja na injini mbili ya kwanza ni
1300 cc huku ikiwa na teknolojia ya VTEC na nyongeza ya IMA (INTEGRETED MOTOR ASSIT) Kwa nn uteseke sasa kwenye mafuta yaani kama inanusa kidogo tu .....
Injini ya pili inakuja na cc 1500 bado ni rafiki sana kwa mtumiaji yaani haikutoi jasho katika mafuta huku ikiwa na technolojia ya VTEC +IMA
Transmition sasa imekaza hatari 7 speed automatic huku ikiwa na chaguo moja tu 2WD Kwenye miguu yake
Njoo sasaa uangalie grade za gari hii kwa nini usiimiliki ? Jaman
2012 Honda Insight Grades
##Honda Insight G – Hili ni toleo zuri sana linakuja na injinj ya cc 1300( 1.3L) huku ikiwa na 15-Inch steel rims, key entry + start, clothe seats, CD/Radio player na halogen headlights....na kuifanya ionekane ya kishua sana kama unatakanuber au tax hili toleo litakufaa sana
##Honda Insight L – Hili ni toleo linakuja pia na injini ya cc 1300 (1.3L) huku ilitofautiana kidogo na na toleo huku gari ikiwa na 15-Inch steel rims, smart key, clothe seats, DVD Player, xenon headlights, rear camera na auto tailgate.
## Honda Insight Exclusive XG – T)Hili ni toleo linakuja na injini ambayo ipo fiti kwenye mwendo cc 1500( 1.5L )huku gari ikiwa na 15-Inch steel rims, key entry + start, clothe seats, CD/Radio player na halogen headlights.
## Honda Insight Exclusive XL – Hili ni toleo ambalo ni luxury grade ni zurri sana kwa matumizi ya familia na linakuja na injini ya cc 1500( 1.5L )huku ikiwa na , 16-Inch alloy rims, smart key, vinyl seats, DVD player xenon headlights, paddle shifts, rear camera na auto tailgate.
## Honda Insight Exclusive XL Inter Navi Select – Hilinpia ni toleo ambalo ni luxury grade na linakuja naninjininya cc 1500(1.5L) huku kukiwa na utofauti kidogo wa vitu km 16-Inch alloy rims, smart key, vinyl + clothe seats, DVD/Navigation system, xenon headlights, paddle shifts, rear camera na auto tailgate.
Upande wa mafuta vipi ??? Yaani hapa unaweza kuzimia lakini ni ukweli mtupu honda hawana utani yaani hii hata kama ni mwanachuo ukinunua hakuna mawazo ya wese
Upande wa ndani
Gari hili limesanifiwa vizuri ,viti vinampangilio mzuri sana honda hawajawahi kukosea kabisa …..upande wa mbele legroom ni kubwa hata kwa nyuma viti viwekwa vizuri kuna door panel,cup holder hivi vitu unavipata katika gari hili ni gari standard sana
2012 Honda Insight Fuel Consumption
2012 Honda Insight 1.3L cc1300 inatumi km 31.0 kwa lita 1
2012 Honda Insight 1.5L cc1500 inatumia km 26.5 kwa lita 1
Wewe endelea kudanganywa na fundi wako wakati honda ni brand kali
[emoji746]2012 Honda Insight Acceleration
[emoji746]2012 Honda Insight 1.3L accelerates kutoka 0-100 km/h kwa11.5 sec.
[emoji746]2012 Honda Insight 1.5L accelerates kutoka0-100 km/h kwa9.8 sec.
[emoji3533]Tank lake ni lita 40 ,ukiweka mafuta full mpk miez miwili ikate ndio tank linaisha full kula vichwa na misele
[emoji3533]Other Extras: Paddle shifts, USB Charging Port, Reverse Camera, Alloy Rims, ECO Assist
[emoji3533]Safety Features: SRS Airbags, Curtain airbags, ABS, VSA, Front Active Headrests, TRC
GROUND CLEARENCE NI 5.7 INCH
Hapa honda wamenihuzunisha uvungu mfupi kwa baadhi ya njia inabidi kulipeleka taratibu sana lisikwaruze ....ikama unataka kulitumia maeneo ya kijijini unaweza kuliinua kidogo kwa kufata kanuni salama kbs bila kuathiri ubora wa gari nione nikushauri ila unanilipa ukija mesenger ...[emoji847][emoji847][emoji847] ila ni bonge la gari inafaa sana tena sana ...but you can change the size of tyre
Upande wa spare
Spare zake kwa sasazinapatikana ukienda pale ilala boma kwa TRANS mathias spare parts unapata spare nyingi ila bei yake imechangamka kidogo ila changamoto ni. Betri yake ya hybrid ikifa ukiagiza mpk unaipta lazima ikugharimu sh Milion 1.5 ,Ila betri yake inachukua mika mpk 6 au 7 kuharibika ni betri imara sana..ambalo limeundwa kwa material ya maalumu tofauti na betri za kawaida ...usiipime gari ubora kwa upatikanaji wa vipuli
SPARE ZAKE INA SHARE NA TOYOTA PURIC C AMBAYO NAYO NI HYBRID ...hapa wajapani waliunda gari moja kwa kushirikiana halafu wakzipa majina tofauti lengo ni kunasa wateja hii ni mbinu wamekuwa wakiitumia sana
Kwani ununue hii gari
1. Exceptional fuel economy
2. Practical and functional
Nisichopenda
Betri yake ya hybrid ni ghari sana kuinunua hasa unapota kufanya miss placement na nyingine...ni muhimu kuzingatia namna ya utunzaji na kufanya service kwa wakati ,na nimuhimu anayefanya mara kwa mara akague kwa kutumia dignosis machine itakusaidia sana gari hili lidume
Mwisho
Ukitaka kununua gari hebu ziba masikio halafu fanya maaamuzi ...achana na walioshindwa wanamaneno mengi hawataki kurudi shule kujifunza kuhusu hybrid ,Yaani watachemka sana…….ni gari nzuri kwa dunia ya leo haina kelele kabisa yaani unaweza kumfumania hata wife na mchepujo unaingia mpk ndani hajui kama umekuja na gari
Kuna watu wanapenda sana kukatisha tamaa hasa manazi wa Toyota walio jf tubadilike
[emoji120][emoji1241][emoji3581]Umemaliza kila kitu.
Unafaa kuwa marketing manager wa hizo gari.
Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
Lakini kabei kamechangamka kidogo.[emoji120][emoji1241][emoji3581]
Nje mada kidogo. Nimetokea kuipenda sana Toyota Prius kwa mwonekano wake. Vipi unajua ulaji wake waafuta ?Ngoja waje wakupe muongozo vizuri ila nachofahamu hii gari ni hybrid kama ilivyo toyota prius
Soma maelezo yangu hapo juu kila kitu kipoNje mada kidogo. Nimetokea kuipenda sana Toyota Prius kwa mwonekano wake. Vipi unajua ulaji wake waafuta ?
OEM au Aftermarket?Honda ni gari nzuri sana. Tatizo kuu ni upatikanaji wa vipuri ni tatizo kubwa sana.
Spear za honda ni issue. Unaweza kudhani Honda wanatengeneza spear chache ukilinganisha magari wanayotengeneza.