Naomba ufafanuzi wa uhalali wa mafao kwa mwanandoa Mwenza

Naomba ufafanuzi wa uhalali wa mafao kwa mwanandoa Mwenza

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
1,222
Reaction score
776
Naomba kupata ufafanuzi wa yafuatayo,

Nina kaka yangu ana mke wa ndoa na wameshaishi na mke wake kwa miaka 30. Huyu bwana anafanya katika taasisi moja ya fedha mjini Mwanza.

Bwana huyu ana mwezi sasa tokea astaaf hivyo anasubiria mafao yake. Familia yake iko mjini Tanga ila cha ajabu plan zake ni kwamba akishapata mafao aoe mwanamke mwengine na aachane na huyu wa zamani. Shida tunayoina ni kwamba huyu bwana pesa ikishaisha atarudi kwa mke wake.

Swali, je huyu mke ana uhalali gani kisheria ku intervene mafao ili huyu bwana asitapanye?

Swa
 
huyo mpya mafao yakiisha anaondoka kweli umuache mke wa 30yrs for that one?
 
huyo jamaa ni mpumbavu sana na atakuja kujuta
 
Mafao ni haki ya mfanyakazi kwani ni kiinua mgongo chake.
Lakini kwa busara ya kawaida inapaswa familia ifaidike na mafao hayo.
Njia pekee ya huyo mke kupata au kufaidi mafao hayo ni kumshawishi au kuomba msaada wa kisheria wafungue Joint Account ili fedha ziingie humo. Hili litafanya mmoja asiweze kutoa pesa bila kuwa na mwenzake.
Kumbuka huyo bwana ataendelea kupata pensheni yake ya kila mwezi na hii haitaingia Joint Account.
 
Asante sana, hata sisi tunaangalia ile lamp-some na siyo pension ya kila mwezi. Kama kuna uhalali kisheria wa yeye kuingilia kati ili wafungue joint account basi sawa. Asante
 
Back
Top Bottom