Naomba ufafanuzi

BRO LEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2011
Posts
830
Reaction score
603
Habari wana jamvi, naomba ufafanuzi wa kisheria kwa jambo hili.
Bwana X aliomba mkopo wa benk kwa dhamana ya nyumba ambayo ilikuwepo eneo ambalo halijapimwa na viongozi wa mtaa wakadhibitisha hati ya mauziano kisha bank ikatoa mkopo.
Bwana X akashindwa kulipa mkopo wake bank ikaikamata kupitia dallali na kuuza kwa mnada wa hadhara.
Baada ya mauzo na aliyeshinda tuzo kulipa alilabidhiwa na bank ile hati ya mauziano iliyow3kwa dhamana.
Bwana X akagoma kutoka kwenye nyumba kwa misingi kwamba eneo hilo lilishapimwa na ana hati ambayo ameiweka dhamana kwa mkopo wa taasisi nyingine.
Sasa hapa napenda kufahamu haki ya msindi wa tuzo ya mnada itakuwaje, na je iwapo mwenye dhamana ya hati halisi ya kiwanja akijitokeza itakuwaje.
N..B. Bwana X alitengeneza hati na hakutoa taarifa kwa bank ya awali.
Asanteni mawakili wasomi na wanasheria.
 
Watu wa sheria watakuja kutoa ufafanuzi.

Ila kwa uelewa wangu mdogo, benki haikupaswa kutoa mkopo bila ya kutokuwa na hatimiliki halisi ya nyumba. Hilo ni kosa la kwanza.

Kosa la pili, ni benki kupiga mnada na kuuza nyumba kwa mtu mwingine bila kuwa na hati. Na huyo mtu naye akajaa kingi. Kosa la pili.

Kiuhalisia mwenye uhalali wa nyumba ni yule mwenye hati halisi.

Sasa mshindi wa tuzo anapaswa kuishtaki benki kwa kumuuzia nyumba isiyo yao. Kisha benki nao watajua namna gani watambana jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…