KWenu wataalam wa lugha, huwa ninapata wasiwasi kidogo ninaposoma habara kama 'lori la mizigo limepata ajali' au 'basi la abiria'. Kwa mtazamo wangu ninaona mtu akishasema tu lori inatosha na hakuna maana ya msingi ya kuongeza hayo mengine kama la mzigo maana katika mazingira ya kawaida hatutegemei kusikia lori la abiria ingawa sehemu nyingine lori linaweza kutumika kubeba abiria. Ninaomba kusikika kwa wataalam wa lugha.