Naomba Ufafanuzi

Naomba Ufafanuzi

Mtumishi Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
259
Reaction score
92
KWenu wataalam wa lugha, huwa ninapata wasiwasi kidogo ninaposoma habara kama 'lori la mizigo limepata ajali' au 'basi la abiria'. Kwa mtazamo wangu ninaona mtu akishasema tu lori inatosha na hakuna maana ya msingi ya kuongeza hayo mengine kama la mzigo maana katika mazingira ya kawaida hatutegemei kusikia lori la abiria ingawa sehemu nyingine lori linaweza kutumika kubeba abiria. Ninaomba kusikika kwa wataalam wa lugha.
 
Hapa ni semantics tu mkuu. Lakini kuna tofauti:

Basi lisilokuwa na abiria likipata ajali ni kitu kimoja.
Lakini basi lililojaza abiria likipata ajali ni kitu kingine.

Lori lisilokuwa na mizigo likipata ajali ni kitu kimoja.
Lakini lori lililosheheneza mizigo (kama mafuta - petrol) likipata ajali ni kitu kingine kabisa.

Wape waandishi uhuru wa lugha mkuu.
 
Back
Top Bottom