Naomba Ushauri: Gari gani linamfaa mstaafu.

Rchesse

Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
60
Reaction score
28
Mama yangu ni mwalimu na anastaafu mwaka huu, na alikuwa anafikiria kununua gari. Kati ya haya lipi unaona linamfaa kwa budget isiyozidi 18M?. Mimi nilikuwa nafikiria haya, unaweza kuongeza unayodhani yanafaa zaidi.

Forester 2007 (najua 08 ndio bora zaidi lakini budget ndio tatizo)

Nissan xtrail.
 
Mstaafu gari ya nini? Atafanyaje mazoezi ya kutembea? Au atojoin na gym pia?
 
Hatujajua Mazingira aliyopo ni Town au Bush na Matumizi yake sana sana ila naunga mkono Rav 4

Yupo mji mdogo, matumizi yake ni kwenda sokoni, kanisani n.k labda ikitokea na safari ndefu ya kwenda kwao na familia kilometers kama 700 hivi.
 

Ili watu wakushauri vizuri, ungeweka wazi matumiza ya gari unalotaka kununua, mfono biashara, matumizi binafsi/kutembelea n.k.
 
Mstaafu gari ya nini? Atafanyaje mazoezi ya kutembea? Au atojoin na gym pia?

Siku nyingine atakuwa analiacha, pia anapenda kujishughulisha sana, kama sahivi anatembea km 2 kwenda kazini na kurudi.
 
Ungefafanua,hanampango wakilimo trekta inamfaa sana,pengine ingepiga hiyokazi na akaja akanunua gari baadae..(nipotayari kua msimamizi wahiyo treka shamba)..kikubwa mkataba uwe soft
 
Huu ndiyo ushauri bora kabisa maana kwanza gari ni gumu na vipuri vyake ni bei rahisi, lakini pia akiamua kuliuza ni fasta sana

Asante kwa ushauri tutajadili hili pia.
 
Ungefafanua,hanampango wakilimo trekta inamfaa sana,pengine ingepiga hiyokazi na akaja akanunua gari baadae..(nipotayari kua msimamizi wahiyo treka shamba)..kikubwa mkataba uwe soft

Hapana mkuu hana mpango na kilimo atafanya shughuli nyingine.
 

Bi Mkubwa anataka gari akiwa ni mstaafu je ataishi mjini au shamba? je atakuwa anasafiri nayo mbali au atapigia misele town? je baada ya kustaafu atategemea pensheni tu au atakuwa na njia zingine za kuongeza kipato? je ana familia ya ukubwa gani? lakini kwa mie vyovyote iwavyo "TOYOTA" inabaki kuwa bora number moja hasa Rav4, Noah Liteace (sio Voxy kimeo), Raum, Starlet, IST, Allex, Fielder, Runx na zinginezo zote familia ya Corolla kwani hatajutia matumizi ya mafuta, upatikanaji wa spare, Bei rahisi kwa vipuri na hata mafundi wa gari hizo ni wengi hivyo hawezi kukwama porini
 

Itakuwa ya misele town kama kwenda kanisani, sokoni, kwenye vyama n.k. pia safari ndefu za kifamilia. Familia ni ya watu 4 nayeye wa 5 ila muda mwingi wengi hawapo. Atakuwa na njia nyingine za kujiingizia kipato. Rav 4 old model ina Cc ngapi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…