Naomba ushauri; hiki ninachoenda kufanya ni sahihi?

Naomba ushauri; hiki ninachoenda kufanya ni sahihi?

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Wakuu habari zenu na poleni kwa majukumu.

Naombeni ushauri kwa hili jambo ingawa ni la kiofisi ila naamini humu nitapata muongozo au mawazo yatayoniongoza kufanya maamuzi sahihi.

Ipo hivi, nipo kwenye kampuni ambayo inajihusisha na mambo ya afya narudia tena (a profit kampuni) kwasasa nimepewa kusimamia jukumu la kuhakikisha funds zinapatikana kwa ajili ya kuongeza wigo wa huduma na moja ya sehemu tunazotoa huduma ni kwenye vituo vya afya vya serikali vijijini na ni bure kwa vituo vya serikali tu.

Njia rahisi niliyoiwaza ya kupata pesa na kutunisha mfuko wa kampuni kwa ajili ya huduma tunayotoa ni kupitia fundraising kwa hivi vituo vya afya vya serikali ambavyo tunatoa huduma bure.

Moja, ninachouliza ni sawa kufanya fundraising kupitia kampuni, maana sisi sio NGO.

Pili, kabla sijafanya maamuzi ya kupeleka wazo hili kwa mkuu wangu unanishauri njia gani nyingine ya haraka ya kupata mapato kwa huduma tunazotoa bure kwa serikali?

Naombeni ushauri wenu na uzoefu wenu wakuu
 
Mimi ni mtaalamu wa afya lakini pia project planner wa siku nyingi nicheki dm nikupe ideas za kutosha nicheki dm
 
Back
Top Bottom