Huu ni ugonjwa hasa kwetu hapa tanzania, wengi huwa wanafaulu vizuri ila hawana elimu ya faculty. Na hii hupelekea wengi kusomea vitu wasivyo vipenda matokeo yake hata ufaulu huwa mdogo, kwani hiyo fani haiko moyoni. Mfano wengi hujikuta wanasomea education pasipo kutaka, simply wameshauriwa hivyo, au hata kulazimishwa.
Nini cha kufanya: elimu ya faculty itolewe advanced level, au kuwe na hata vipeperushi vya faculty na point pia ukiisoma utakuwa nani, (utapata ajira gani) ili mtu asome na achague mwenyewe.
Kuhusu muuliza swali: Fanya yafuatayo:-
1. Angalia ufaulu kwa kipindi hiki je, ni mkubwa au ni wa kawaida. kama ni wa kawaida apply vyuo vya kawaida na visivyo na majina makubwa
2.usikilize moyo wako unataka nini na ungependa uwe nani katika maisha yako (kazi uipendayo na unayohisi utaiweza).
3 fuatilia lengo/ndoto zako,
kwa ufaulu wako tofauti na kuapply education, achana na vyuo vikubwa vyenye majina sana, kama ud, mzumbe, udom, na vinginevyo.
Apply kama sauti, na vinginevyo utapata na utashughulikia ndoto zako.
Pia fahamu soko la ajira haliangalii umesomea wapi, ila unanini kichwani.