Naomba ushauri jinsi ya utiaji wa mbolea katika mche

Ndara Mbovu

Senior Member
Joined
Feb 28, 2017
Posts
155
Reaction score
83
Nimelima matikiti maji kwa mara ya pili sasa, changamoto yangu juu ya utiaji wa mbolea ya viwandani katika miche.

mana inakufa sana nikishatia mbolea.

Natumia kizibo cha take away kama kipimio katika kila mche na naweka sentimeta 5 kutoka kwenye mche, naifukia.

Nilikuwa na miche elfu 5 shambani sasa hivi imebaki elfu 3.8
 
Hongera kwa kuamua kulima ila pia pole kwa changamoto iliyokukuta

Inavyoonyesha kwa hiyo picha hapo juu unawahi kuweka mbolea subiri kwa muda kidogo mmea uzoee hali ya mazingira ya eneo husika alafu wekea mbolea baadae

Ushauri usiwahi kuweka Mbolea kabla mmea haujakomaa
 
Ila naomba kujua tunaweka mbolea ya kukuzia kwe matikiti maji baada ya muda gani toka kupandwa?
 
Kwani Umetumia mbolea gani? Shida sio size ya mmea.Binafsi hua naweka mbolea mara3 kutoka mche hadi kuvuna: Awamu1:Mmea(mche)unakuwa unaweka jani la kati(DAP,NPK-yaramila winner)
Awamu2:Mmea unajiandaa kuweka maua(CAN/CAN+DAP mix)
Awamu3:Mmea umeweka matunda(CAN/mixer)
Kipimo cha mbolea na distance upo sahihi ila kumbuka kumwagilia maji yakutosha Mara baada ya kuweka mbolea
 
Furthermore Jaribu kuchunguza ndani ya udongo huenda kunawadudu wanatabia ya kufyonza majimaji kwenye mizizi ya Mmea was tikiti.....Hii nimeexperience hasa ikiwa shamba linaunyevunyevu mwingi ndo wadudu hupendelea sana
 
Furthermore Jaribu kuchunguza ndani ya udongo huenda kunawadudu wanatabia ya kufyonza majimaji kwenye mizizi ya Mmea was tikiti.....Hii nimeexperience hasa ikiwa shamba linaunyevunyevu mwingi ndo wadudu hupendelea sana
Nashukuru kwa ushauti wako, ngoja nikachunguze.
 
Braza inafika wiki sasa na siku 1 naona bado inakufa, mbolea niliyoiweka nilichanganya kilo 15 za urea, kilo 10 za DAP na kilo 5 za SA, maji namwagilia kwa mitaro kama hvyo kunarowa kweli.
 

Attachments

  • IMG_20181007_111402.jpeg
    108.1 KB · Views: 55
Urea inahitaji uangalifu sana kwani usipo kuwa makini utachoma mimea sana. Weka mbolea kama DAP+ NPK, na CAN wakati wa kuanza uzazi kwa mimea
 
mbolea uliweka mda gani?

maana mbolea za viwandani sharti ziwekwe jioni angalu kuanzai saa 11 jioni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…