Naomba ushauri juu ya biashara ya barber shop

Naomba ushauri juu ya biashara ya barber shop

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Habari za muda viongozi.

Ningependa kupewa dodoso juu ya biashara hii ya vinyozi.

Nahitaji kujua kiwango cha chini cha gharama ya kuanzisha huu mradi, kwa sababu nataka nimfungulie kijana ambae ndio kinyozi mwenyewe, apate japo shughuli ya kufanya. Mimi nikiwa kama mmiliki wa mradi huo.
 
Shukrani.

Hapo hapo ningependa nijue tofauti ipo wapi kwenye hizo za 5M na 2M.
Yani vitu gani vinaongezeka au vinapungua kati ya hizo mbili.
Ya 2M ina viti vya kawaida visivyozidi vinne... Inakuwa na feni tu na haina zile huduma za ziada
Ya 5M+ ina AC, viti vya sofa visivyozidi vitano na huduma za ziada

Jr[emoji769]
 
Imekaa poa pia

Kama za kitaa so simple mkuu
1.Vioo vikubwa viwili sheet nzima k.koo 40k bila alminium, ukiweka na alminium kimoja kinafika mpka laki(kubana bajeti unaweza nunua sheet moja ukakata kati ukaweka frem za mbao km design)
2.Feni ya juu k.koo50-70
3.Sofa moja120
4.Mashine mbili, imara homecut og 120-150, bt zipo had za 80-100 hata za 30k bt ukinyolea watu wawil zimeshika moto
5.kuweka mlango wa alminium(sio lazma , ckuhz wanaweka pazia tu za kamba)
6.Kiti cha kunyolea 80-180
7.Dustbin,fagio,vitambaa,poda,etc-50
6.Sabufa,sio lazma
7.Taa kubwa -10k

Mengne mbwembwe ila had hapo unaweza kumpa kijana akapia kaz
 
Nilifunguaga saluni yangu baada ya kumaliza kitabu nikawa napiga mwenyew likizo nilipoendelea nikaweka mtu ndo akaniharibia biashara anakuja kalewa hesabu hatoi nikafunga vtu vpo home natuliza akili nitafute location na kijana

God bless kama umeamua fanya hvyo
Baada ya hapo gharama hakuna zaid ya kodi,umeme na viwembe
 
Uzuri kijana ni wangu. Akinizingua kwenye hesabu, ndio anakua kajiharibia mwenyewe. Mimi napiga chini tu!
 
salun ya kiume ya kisasa n kuanzia 8m na kwenda juu...kiti kmoja n kuanzia 800k, mashine ya kunyolea ord 120k, bado udambwi udambwi mwingne.
 
Nilifunguaga saluni yangu baada ya kumaliza kitabu nikawa napiga mwenyew likizo nilipoendelea nikaweka mtu ndo akaniharibia biashara anakuja kalewa hesabu hatoi nikafunga vtu vpo home natuliza akili nitafute location na kijana

God bless kama umeamua fanya hvyo
Baada ya hapo gharama hakuna zaid ya kodi,umeme na viwembe
Hesabu ni sh.ngapi kwa siku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barbershop nzuri kwenye location inayolipa haitapungua 10,000,000. Narudia tena kwenye location inayolipa, lakini kama ni location yoyote tu hapo gharama zinapungua sana.

Barbershop za siku hizi zinahitaji space ya kutosha, hivyo Kodi inaweza kuchukua kiasi kikubwa kama hutafanya utafiti wa kutosha.

Changamoto kubwa kwa barbershop ni yule unayempa jukumu la kusimamia, hutapata pesa kwa wakati, it's annoying ilà ndio hivyo vijana wengi hawana focus. Ndio maana nataka niuze niliyonayo.
 
Duh kumbe vijana wanasumbua sana.
 
Duh kumbe vijana wanasumbua sana.
Biashara ya Salon ni nzuri sana ukisimama mwenyewe, nimewahi ifanya hii biashara nikamkabidhi jamaa ofisi. Mwezi mmoja wa kwanza kila kitu kilienda sawa, baada ya hapo mapicha picha yakaanza. Mara leo wateja hakuna, mara wenzangu wamegoma kulipa hela ya umeme, daily sababu zikawa hazikosi. Nikaona isiwe shida nikamtimulia mbali nakuuza vifaa vyangu.
 
Back
Top Bottom