Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Naomba ushauri juu ya biashara ya Uber, Bolt

Baba Richard

Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
24
Reaction score
57
Guys natamani sana kuifanya hii biashara ya Tax kwa njia ya mtandao kama vile kupitia Uber na Bolt lakini sijui ijui sana bishara hii, mwenye kufahamu lolote kuihusu hii biashara anipe info’s kidogo. Ninachotaka kukifanya ni kuchukua gari ya mtu na kuifanyia hiyo kazi kwa hesabu au mkataba. Naomba kufahamu yafuatayo;-

[emoji117]Je inalipa?

[emoji117]Ina changamoto gani na gani?

[emoji117]Kwa siku mtu anatakiwa apeleke hesabu kiasi gani?

[emoji117]Kama gari umechukua ya mkataba mara nyingi inachukua kiasi gani per day na inakuwa ni kwa muda gani hadi iwe yako?

[emoji117]Muda mzuri wa kufanya biashara ni upi na upi?

[emoji117]Ni wapi gari inaweza kupatikana kwa urahisi?

[emoji117]Ni gari gani nzuri kwa ajili ya biashara hii?

[emoji117]Nijiandae na mambo gani strange kwenye hii biashara?

[emoji117]Chochote ambacho sijakiandika hapa lakini unaweza kunishauri?

[emoji117]Link ya uzi wowote kuhusiana na hii biashara kama umewahi kupostiwa humu ila uwe recently

NB: Napokea maoni yoyote yawe positive au negative, Japokuwa watu wenye uzoefu wa muda mrefu itakuwa njema sana kama wakisema chochote kitu kuihusu hii biashara.

Natanguliza Shukarani WanaJF [emoji120]

Zaidi soma:
 
Masengenyo ya Shemeji yamekuchosha eeh. Ningekua wewe Ni mm ningeenda physically ofisini kwao. Badala ya kuuliza mitandaoni
Nimewahi kwenda ofisini kwao na ninajua vigezo vyao, what I wanted to know, sijui kama umeisoma hiyo thread na kuielewa vizuri ni kutaka kufahamu experience ya biashara yenyewe, hiki ni kitu ambacho hawatoweza kukushauri unbiased kwasababu wao wapo behind the desk kumonitor mambo ya IT na Management kwenye kampuni yao.

Ninachotaka kujua hapa ni kwa mtu au watu (Dereva au Madereva) ambao wameifanya hii biashara wakaona in and out ya biashara yenyewe.
 
Nimewahi kwenda ofisini kwao na ninajua vigezo vyao, what I wanted to know sijui kama umeisoma hiyo thread na kuielewa vizuri ni kutaka kufahamu experience ya biashara yenyewe, hiki ni kitu ambacho hawatoweza kukushauri unbiased kwasababu wao wapo behind the desk kumonitor mambo ya IT na Management kwenye kampuni yao. Ninachotaka kujua hapa ni kwa mtu au watu ambao wameifanya hii biashara wakaona in and out ya biashara yenyewe.
Utakuta na wewe unajiita Graduate kumbe kichwani empty set. Endelea kula kwa Shem
 
Utakuta na wewe unajiita Graduate kumbe kichwani empty set. Endelea kula kwa Shem
Kuwa Graduate haimaanishi umegraduate katika maisha.

Baba Richard anahitaji kujua experience kwa waliowahi kufanya hii biashara. Kwenda ofisini kwao haiwezi kumsaidia kupata anachokitaka .

Hebu jaribu kwenda ofisi za Forever Living uone watakavyokupamba, halafu njoo huku mtaani na hiyo biashara uone utakavyosaga soli.
 
Mm nimewah tumia bolt kama abiria, ni cheap sana baada ya kumaliza safar zangu nikapata kumuhoji dereva wa bolt, ilikuwa ni boda kuwa unapata faida?

Alichonijibu ni kuwa hii kazi bro ni nzur kwa sababu si sawa na kukaa kijiweni na kusubir mteja, mfano mm nimekuleta hapa mbagala ww, hapa mm sirud mtupu, program inanitafutia abiria ambae anatoka mbgla hapa kwenda sehemu nyengine, kwa hyo kutwa nzima kazi ipo hvyo hadi inafikia hatua una log off ww mwenyewe, kwa sababu usipokuwa makini utakesha!

Kutwa nzima , nikamuuliza kuhusu malipo akasema mfano kwenye hii 18000 yao jamaa ni kama 1000 au 1500 , so nilichojifunza kutoka kwa yule dereva kutokana na maoni yake ni profitable business kwa upande wake!! Ndio hvy ndg.
 
Bolt ndio iko cheap zaidi na ina ofa sana kwa wateja na wengi wanatumia hiyo kuliko Uber, madereva wanazo hizi apps zote. Madereva wa Bolt wanaingiza hela nyingi kuliko wale wa vijiweni. Yani hujutii kuilipia, uzuri wake kuna siku unapiga kazi mpaka unaamua kupumzika.

Wapo watu anafanya kazi mchana, jioni anapiga Bolt mpaka saa tano usiku anarudisha kagari kake kazuri nyumbani anapumzika. Mmoja alinambia hela ya kula na bills zote nyumbani anaipata kwenye Bolt, mshahara wake haulishi familia hata siku moja.
 
Bolt ndio iko cheap zaidi na ina ofa sana kwa wateja na wengi wanatumia hiyo kuliko Uber, madereva wanazo hizi apps zote. Madereva wa Bolt wanaingiza hela nyingi kuliko wale wa vijiweni. Yani hujutii kuilipia, uzuri wake kuna siku unapiga kazi mpaka unaamua kupumzika.

Wapo watu anafanya kazi mchana, jioni anapiga Bolt mpaka saa tano usiku anarudisha kagari kake kazuri nyumbani anapumzika. Mmoja alinambia hela ya kula na bills zote nyumbani anaipata kwenye Bolt, mshahara wake haulishi familia hata siku moja.
Stori za vijiweni hizo. Uber ndo mpango mzima ila maumivu Yake utayapata siku ya kufanya service kubwa. Pia abiria wake kichomi Sana
 
Back
Top Bottom