cold water
JF-Expert Member
- Oct 6, 2021
- 238
- 954
Nasumbuliwa na mgongo ni takribani miaka mitatu sasa,hasa wakati wa usiku nimekuwa ni mtu ambaye sifurahii sana usingizi,mgongo una asili ya moto tu mda wote na kama sio kuhisi nimepakwa pili pili na kifua kwa mbali kinapataga moto,niliwahi Pimwa vidonda vya tumbo nikaambiwa majibu yako positive nikaanza dawa,nimetumia heligo kit kwa miezi miwili lakini nilipata nafuu tu sio kupona,nilivyoona nakunywa dawa bila mafanikio nikaamua kuacha kabisa dawa,lakini mgongo ukaendelea kuwa na maumivu makali nikaamua kufanya x ray pia ikaonekana kuna tatizo pia nikapewa amox clav,lakini sikuandikiwa na daktari aliandika mtu wa x ray baada ya kugundua tatizo, nikanywa lakini hadi Leo sina nafuu yeyote ile zaidi ya maumivu.naomba uni pm kwaajili ya kunipa ushauri zaidi.Asanteni....