Naomba ushauri juu ya mkataba huu wa ajira na jinsi ya kudeal na muajiri huyu

Naomba ushauri juu ya mkataba huu wa ajira na jinsi ya kudeal na muajiri huyu

Lukumburu

New Member
Joined
Jul 23, 2026
Posts
2
Reaction score
0
Habari za leo wakuu?

Kwa wale wataalamu wa taratibu na sheria za ajira za Tanzania naomba ushauri juu ya muajiri huyu na ni hatua zipi kama muajiriwa napaswa kuchukua kabla ya kusaini mkataba wa aina hii ?Na endapo nitasaini na stahiki zipi nastahili kupata baada ya kipindi cha mkataba huu kuisha?

Historia:

Niliajiriwa kwa mkataba wa kudumu yaani permanent contract ndani ya miezi 6 muajiri akabadilisha mkataba kutoka permanent kuwa fixed term wa mwaka mmoja (12 months).{Ulioanza 1 October 2024 na kuisha 30 September 2025}

Baada ya mkataba wa miezi 12 kuisha muajiri akatoa mkataba wa fixed term tena ila awamu akatoa wa 6 months {Kuanzia 01 October 2025 na ukaisha 31 March 2026}

Baada ya mkataba wa miezi 6 kuisha hakutoa notice ya kusitisha mkataba wala kuextend nikaendelea na kazi huku nikisisitiza kupewa mkataba mwingine.

Ikapita miezi mitatu (3) nikifanya kazi bila ya mkataba wowote ,baada ya kuzidisha kudai mkataba au notice of extension muajiri kaamua kutoa 3 months employment contracts (Kuanzia 1st July hadi September mkataba huu ametoa katikati ya July ila anatoka usomeke kuanzia 1st July) akiterm kama ameniajiri kama temporary employee kama kipengele hiki cha mkataba kinavyosema

********************************************************************************

XXXXX CO LTD hereby appoints the Employee as Short Term Domestic Ops Contractor, Dar es Salaam, on a fixed-term temporary basis commencing on 1 July 2026 for 3 months.

This Agreement is entered into for a short-term temporary requirement only. The Employee acknowledges and agrees that this Agreement shall automatically expire in 3 months without the need for notice of non-renewal and shall not be renewed, extended, or converted into permanent employment.

No verbal assurance, email, message, continued work, payment, conduct, or business requirement shall create any right, expectation, or entitlement to renewal, extension, confirmation, or permanent employment. Any further engagement after the expiry date shall require a fresh written agreement signed by both parties before the expiry of this Agreement
.

**************************************************************************

Vipengele vingine vya mkataba

TEMPORARY PERIOD


4.1 The Employee is engaged for a fixed temporary period only and shall not be subject to confirmation into permanent employment. The Employer may assess the Employee’s performance during the term, but such assessment shall not create any expectation of renewal, extension, confirmation, or permanent employment

PERFORMANCE OF DUTIES

The Employee further agrees to perform all those duties and functions that may be reasonably expected from the position for which the Employee has been engaged in an efficient, trustworthy, professional manner and to the best of his ability, to comply with local laws and in a manner appropriate to the country of Tanzania.

FLEXIBILITY

6.1 The Employee shall have no right to have any other jobs, whether part-time or full-time, or honorary posts without Employer’s prior written permission.

6.2 The Employee shall from time to time be required to perform duties in addition to those associated with his position.

6.3 The Employee may be required to undergo training, necessary to perform certain duties, and the Employee shall have the obligation to participate in such training.

WORKING HOURS

The Employee’s ordinary working hours, shall be from 09:00am to 05:00pm, Monday to Friday. In order to conform with the Employee’s business requirements and the Law, the Employer shall have the right from time to time to change the Employee’s ordinary working hours and break times, including determining Saturday and Sunday and public holidays as working days provided that it complies with the Tanzanian Labour Laws and Regulations.

Kwa kuzingatia mlolongo huo ni hatua zipi napaswa kuchukua na maslahi yapi nastahili kupewa ukizingatia kwa kipindi chote sijawahi kwenda likizo yeyote rasmi toka nimeajiriwa.

Na pia kama nitakubaliana kuachana na huyu muajiri ukizingatia nimekua nikichangia pension NSSF mkataba huu wa mwisho utakuwa na impact zipi kwenye madai ya mafao yangu.

NB:Muajiri ni kampuni ya wahindi na mimi binafsi nimechoka pia kuendelea kufanya nao kazi kutokana na longo longo ni nyingi..mfano mkataba wa kwanza wa permanent na baadae ukabadilishwa kuwa fixed term una kipengele cha kupewa bima ya afya na commission kila mwezi kutokana na margins produced ila hakuna alichotekeleza hata kimoja zaidi ya kulalamika biashara hailipi huku tukiendelea kuongeza volume ya biashara.

Pia kufanyishwa kazi nje ya muda rasmi wa kazi kama ilivyoainishwa kwenye mkataba kama usiku ,weekend ,public holidays unapigiwa simu na kupewa majukumu muda wowote wanaojisikia wao.

Mmiliki wa kampuni ni mhindi yuko India ndie alieniajiri kwa mara ya kwanza na kunipa mkataba wa kudumu baadae akaajiri wahindi wengine nije kufanya nao kazi hawa wahindi njaa baada ya hawa wahindi kuajiriwa ndio mabadiliko ya mikataba yalipoanza na kutoa mikataba imekua ni ngumu na wengine wanaajiriwa kwa simu na kuachishwa kazi kwa simu pia plus unafiki ni mwingi sana.

Natanguliza shukrani za dhati kwa watakaonishauri na kunipa muongozo yatayolinda maslahi yangu.
 
Back
Top Bottom