Pole
fettydia kwa hofu na wasiwasi ulionao juu ya dalili hatarishi kwa maendeleo ya mtoto aliye tumboni. Fuatilia maoni na ushauri murua wa wana JF na hapana shaka Mungu atakusaidia na hali itakuwa shwari.
Japo upo kwenye wasiwasi na hofu, naomba nami unifahamishe ni dawa gani ulitumia kukuponya maumivu ya tumbo na hatimaye kushika ujauzito? Umesema hapo kabla umesumbuliwa sana na maumivu ya tumbo mpaka ukahisi huna uwezo wa kushika ujauzito.
Mke wangu ana shida kama uliyokuwanayo wewe ya maumivu makali zaidi kuliko kawaida na suala la kushika ujauzito kwake limekuwa gumu licha kufanya vipimo na wote kuonekana hatuna tatizo.
Ahsante.