Na sijajua Mshahara utarudishwa ama la!sa nahofia kupoteza muda wangu hapa alafu iwe bila bila
Ndugu kwanza nakupongeza kwakujiendeleza,kikubwa hapa nakushauri ajira mpya zikitoka wee nenda kapge kazi kuliko kukaa hapo bila kujua hatma yako!
Pili nakushauri kama ukifanikiwa kupata ajira mpya na kuingizwa kwenye payroll bila matatzo ukimalza miaka miwili kazini fanya mpango ukasome masters tena hiyo masters isiwe ya education...mfano kama umesomea kufundisha masomo ya geograph na G.S nakushauri ukapge masters ya HRM (Human Resource Management) au kama umesomea masomo ya economics,commerce na a/c -piga masters ya finance,accounting,procurement,management,project management,au masters ya economics... .
Kama umesomea masomo ya physics unaweza piga masters ya ICT au MBA -ICT,......
Lengo la ushauri wangu nikutaka kukwambia kwamba ualimu haufai kwa hapa Tz!ila utumie ualimu kama daraja lakufikia malengo yako....
★★-
UTAFANYAJE ILI MWAJILI WAKO AKURUHUSU KUSOMEA KITU TOFAUTI NA UALIMU?
...Kwanza,mwajili wako kamwe hatakuruhusu ukasomee kitu tofauti na ualimu. ..ila unatumia akiri yako kumzuga mwajili.....
Unaomba masters unayoitaka(lets say MSc. Accounting )kwenye chuo X (tuchukulie Mzumbe)alafu unaomba master degree ya ualimu kwenye chuo Z(tuchukulie UDSM)...
Unapotaka kuomba ruhusa unaitanguliza admission form ya UDSM yenye koz ambayo mwajili atakupa ruhusa na ile yenye adm form ya mzumbe (yenye kozi uipendayo sasa)unaiminya......
Mwajili akikuruhusu tu,wewe unaishia zako mzumbe!
Ukimaliza tu kupga MSc yako ya Accounting unafanya mpango wakubadilishiwa kaz kwenye halmashauri yako(recategorization) yaani mwajili wako akutoe kwenye kushika chaki akuweke kwenye kushika pesa na cheque!(aaahaaaah) najua umefurahi jinsi move ilivyoenda)..
Na ukiona kwamba mwajili wako anazingua basi hama halmashauri ( tafuta halmashauri yenye wakuu flexible wanaoweza kukubadilishia kaz hata kwakuwatoa mkwanja-bongo rushwa imejaa ukijifanya msafi utashangaa umebaki peke yako kwenye mataa).....
★★-★----------
Onyo.
Usimwambie mtu yeyote hata awe rafiki yako vpi hapo kazin maana walimu wengi (si ajabu na wewe ukawa mmoja wao)wana wivu sana!hawapendi mwenzao apige bao....
Ukiwaambia tu utashangaa majungu na hata ruhusa hutapata(kiufupi utawekewa bams kwa kila ukifanyacho)
★★
Utapata wapi ada yakusoma masters?
Kopa benki.....sio baypot au blue sijui!kule utajuta!utatembea na chupi kichwan kwa jinsi watakavyokutia matatizoni....
Hiz microfinance organs nyingi zinazojinasibu kwamba zinatoa mkopo ndani ya masaa 24 ni wezi...kaa mbali nao!waogope kama ebola ya sieraleon maana kuna ya uganda haina nguvu!(uliona wapi ebola inazibitiwa ndani ya wiki 2 kama si ebola ya uganda?!)
Kakope CRDB,NMB(japo wanalinga na niwaomba rushwa sana-utadhan hawalipwi),Posta bank au NBC....
hizo ndo benki zakukopa.
Ukikopa Milioni 9 tu,utalipa ada full na utabaki na kama 3M zakukusukuma ukamaliza master degree yako bila shida....
NB;- ukikopa fanya ulicholenga!lipa ada! Sio unaanza kumtafuta Fatuma umuonyeshe ulivyomtamu(kama mcharo vile) oooh utajuta na utashangaa ada tu ya 6M inakushinda.
Pia elewa haya yote yanahitaji moyo wakijitoa,ujasiri...moyo wakupambana!laa sivyo utasanda na utakufa kwa chaki....
(Kama una maswali zaidi ni PM)
-★★
Specialist88.