Naomba ushauri kuhusu bati bora na ambayo haipauki

chukua ALAF. huko kwingine ni kujitafutia majuto tu
 
Na kama alaf uende kiwandani kabisa sio kwa wale makanjanja walioko nije ya kiwanda ambao anakuona hata umesimama unataka kuongea na simu wanakukimbilia hao ni makanjanja wa mjini 2 zama ndani ya kiwanda kabisa ila hata sunshade nasikia nao wapo vizuri.
 
Yeah aingie moja kwa moja kiwandani atapata bei nzuri pia, hii ya kutafuta urahisi kwa kutumia madalali ndio wanaishia kulizwa na mabati feki au gharama kubwa kupita kawaida.
 
yeah aingie moja kwa moja kiwandani atapata bei nzuri pia, hii ya kutafuta urahisi kwa kutumia madalali ndio wanaishia kulizwa na mabati feki au gharama kubwa kupita kawaida
Pia asidanganyike na kofia, misumari na usafiri wa bure kwani hizo ndo mbinu wanazotumia kupata wateja si unajua wa TZ wanavyopenda slope pia hata haya maduka ya vifaa vya ujenzi nao ni makanjanja 2 ingawa sio wote.
 
Kila mtu amekariri Alaf na Dragon kama jins watu wengi wanavyoamini kampuni ya Tronic ndio inavifaa bora pekee vya umeme.

Tusikariri vitu,, kuna kampuni mpya ya bati inaitwa POLARIS iko poa kinoma na unachukua mzigo kiwandani pia bei iko vizuri sana, bati imara sana aiseee.
 
yeah aingie moja kwa moja kiwandani atapata bei nzuri pia, hii ya kutafuta urahisi kwa kutumia madalali ndio wanaishia kulizwa na mabati feki au gharama kubwa kupita kawaida
Mimi niko vwawa Mbozi mkoa wa Songwe hakuna kiwanda nitafanyaje mkuu.
 
Pia asidanganyike na kofia,misumari na usafiri wa bure kwani hizo ndo mbinu wanazotumia kupata wateja si unajua wa TZ wanavyopenda slope pia hata haya maduka ya vifaa vya ujenzi nao ni makanjanja 2 ingawa sio wote.
Kabisa mkuu, kwanza kofia anaweza kutengeneza mwenyewe kwa kununua sheet za bati za kawaida tu kisha fundi anaenda kumkatia kofia, bati moja la shilingi 30000 unaweza kutoa mpaka kofia 3 wakati kofia moja wao wanaweza kukuuzia shilingi 22000, misumari pia kama ni ya rangi anaweza kuagiza kilo chache kwanza ikipelea atarudi kuongeza haina gharama kuliko kuagiza misumari mingi mwisho ikabakia akapata hasara. kuhusu usafiri asijali ilimradi amechukua kitu bora kwa bei halisi ya kiwandani. Otherwise slope inaumiza.
 
Inawezekana mkuu lakini watu wanapendekeza ALAF maana hayajawahi kuangusha mtu, kama kuna kampuni mbadala ya ALAF basi ni vizuri washindani waongezeke wateja tupate unafuu wa bei. lakini inabidi tuwape muda hao mbadala wa ALAF tujiridhishe na ubora wao.
 
Kwenye TRONIC napigilia msumari hapo, hakuna kampuni ya vifaa vya umeme iliyo bora kama Tronic. Kama ipo nitajie.
 
Kwenye TRONIC napigilia msumari hapo, hakuna kampuni ya vifaa vya umeme iliyo bora kama tronic. Kama ipo nitajie
Unaposema kuna mbadala lazima uje na mbadala unaozidi kiwango cha ile bidhaa ya mwanzo. Siyo unasema kuna nzuri kama TRONIC alafu kumbe hata haijaifikia wala kuizidi tronic.
 
Kwenye TRONIC napigilia msumari hapo, hakuna kampuni ya vifaa vya umeme iliyo bora kama tronic. Kama ipo nitajie
Apo ndipo mnapoibiwa, mnauziwa vifaa vya umeme vinapigwa lebo ya Tronic basi mnaweka imani kuwa ndio super, Copy ni nyingi saiz.
 
SHORTCUT IS WRONG CUT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…