Naomba ushauri kuhusu bati bora na ambayo haipauki

Naomba ushauri kuhusu bati bora na ambayo haipauki

hivi hii imekaaje Alaf kiwandan ni 470K per bando kwa wakala ni 450K
 
Bati ya ALAF na dragon, ipi bora, na ni ipi ambayo haipauki? Kama kuna anayejua kampunii nyingine, naomba ushauri. Na bei zake
Ni BATI ZA ALAF PEKEE NI NZITO HAZIPAUKI NA ZILE ZA SILVER YAANI CORRUGATED IRON SHEETS HAZIPATI KUTU ASILANI
 
hivi hii imekaaje Alaf kiwandan ni 470K per bando kwa wakala ni 450K
Hizo za kwa wakala huwenda sio za ALAF au Ni rejected kachanganya
BATI ZA ALAF NDIZO BATI BORA MKUU NINA UZOEFU NAZO TAKRIBANI MIAKA 27 NINAITUMIA NA SIJAONA NILIPO EZEKEA ZIMEPATA KUTU AU KUPAUKA
 
Kwenye TRONIC napigilia msumari hapo, hakuna kampuni ya vifaa vya umeme iliyo bora kama tronic. Kama ipo nitajie.
Kuna Philips na Osram hutajuta vifaa vyake mkuu, na bei ni juu kidogo.
 
Jaman namimi naomba msaada wa kujua bati kiboko Gage 28 bei gani kiwandan?na kiwandan kipo wapi hapa Dar?naomba msaada
 
Kila mtu amekariri Alaf na Dragon kama jins watu wengi wanavyoamini kampuni ya Tronic ndio inavifaa bora pekee vya umeme.

Tusikariri vitu,, kuna kampuni mpya ya bati inaitwa POLARIS iko poa kinoma na unachukua mzigo kiwandani pia bei iko vizuri sana, bati imara sana aiseee.
Tayari ushasema kampuni mpya halafu umeshaipa warrant kuwa wako vizuri zaidi ya ALAF... Umeezekea bati zao lini na zina muda gan?
 
Kwa hapa bongo kampuni ni
1: Alaf (nime zi piga sana hazina shida)
2: Sunshare(wako vizuri mno wamezidiana umaarufu tu na Alaf)
3: Kiboko (hawa jamaa wako vizuri ila kunamwaka waliingiziwa material fake hii ndo iliwachafulia jina

4: Sunder(nao hawapo nyuma bati zao nzuri ila kwenye gauge changamoto kidogo)

5: Hando (tangu ianze kutumika Tanzania haina muda mrefu kwahiyo bado sijaona ubora wao mana hata miaka mitatu bado)

6: Bati bomba sijazitumia sanaa

Hiyo Ando ina miaka 10+ na katika kampuni zenye bati quality ni hao jamaa, nimewahi fanya nao kazi, mfano mzuri wameezeka Chamwino Ikulu. fanya research utakuja kuprove, as for ALAF wako poa pia ila kwa hawa wachina wana probability ya 50/50 kwa ubora unaeza pata quality au ukachemsha
 
Kila mtu amekariri Alaf na Dragon kama jins watu wengi wanavyoamini kampuni ya Tronic ndio inavifaa bora pekee vya umeme.

Tusikariri vitu,, kuna kampuni mpya ya bati inaitwa POLARIS iko poa kinoma na unachukua mzigo kiwandani pia bei iko vizuri sana, bati imara sana aiseee.
Habari kiongozi,wewe ni mhusika wa hizo Bati? maana sijawahi kusikia popote zikitajwa na mafundi wa humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom