Pole mkuu, mi nilifumania pesa mwezi wa tatu nikapata bajaji marejesho 20k, nakumbuka pesa ilirejeshwa kwa siku 15 pekee baada ya hapo ikawa marejesho 15k kwa tabu sana.ikabidi Niiuze baada ya kuona mambo yanaenda kufeli, Nikatafuta mwanasheria nikaingia mfukoni akaandika mkataba wa pikipiki, nikaanza na pikipiki 2 mwezi wa sita mwaka huu, sina masihala kabisa na kazi yangu. Mpaka sasa napikipiki nne na mkataba unafuatwa, mkataba unaotambulisha kazi ya boda kama kazi zingine rasmi. Ukicheka na nyani...., ushauri wangu uza hizo bajaji hata mbili baada ya kuwa umezikarabati, then nunua boda afu tafuta vijana wape mkataba halafu JIZIME DATA