Naomba ushauri kuhusu Biashara ya Bajaji

Biashara ya vyombo vya usafiri ni ngumu,mi ninalo guta nimejionea mwenyew hii biashara ilivyo,siwez kumshauri mtu achukue 6 mil zake anunue hili dude

Vyombo vya usafiri inatakiwa ndani ya mwaka mmoja kiwe kimerudisha hela tofauti na hapo utakuwa umeliwa kama kila siku kitakuwa kipo barabarani

Hv vyombo vya usafiri hasa vya kichina baada ya mwaka mmoja kila kitu huwa kinaisha isipokuwa block engine

Hili dude nimeamua kuwa dereva mwenyewe,napiga kazi mara moja moja,kwasasa linaweza kumaliza mpaka miezi miwili pasipo tatzo nabadili oil tu
 
Duh asee guta ndio target yangu january nilinunue, nimeambiwa imara ni wanhoo, hebu nipe abc zake kabla sijaghairi kulinunua.
 
Duh asee guta ndio target yangu january nilinunue, nimeambiwa imara ni wanhoo, hebu nipe abc zake kabla sijaghairi kulinunua.
Kiukwel haya madude inatakiwa kuwa nalo makini sana,mimi nina guta kampuni ya TOYO cc200

NI vzur ukanunua cc200 yana matumiz mazur ya mafuta

Usilipigishe safari ndefu sana zaidi ya km 100 likiwa na mzigo mkubwa

Usitumie ile gear ya high kwa umbali mrefu maana litawah kuharibika kwenye dif

Cc200 uzito wa mzigo usizid tani 1
Oil badilisha kila inapotakiwa

Hakikisha linatengenezwa na fundi anaeyajulia haya madude,sio kila fundi pikpik anajua kutengeneza hz kitu

Usilitumie kwenye njia yenye mchanga mwingi au sehemu zinazotitia likiwa na mzigo

Nikifanikiwa kununua lingine nitachukua WANHOO hata mimi

Uzuri wake likipiga trip moja tu au mbili una uhakika wa kupata hela ya kula
 
Dahh aisee yaliyokukuta wewe, ndo yaliyonikuta mimi, mimi sina hamu na hayo madude, lipo langu nilinunua 2019 mwenz wa 8... Mwaka jana mwenz kama huu wa 12, ikabid tu ninunue engine mpya..ndo hadi sasa linafanya kazi ila body imekufa kbsa, ikitembea makelele tupu..!! Ila nimejifunza meng na hayo madude changamoto zake zimekua fundisho kubwa kwangu, kama mwenyewe una nafasi ni bora uendeshe mwenyewe kwa kijijin litakulipa vibaya sana, ila ukimpa dereva mnagawana tu,
 
Engine zake ni bei gani,maana sahv navyolitumia mimi mwenyew naamin nikipata engine mpya litatulia kabisa,mimi nililichukua 2020 mpaka sasa body liko vizur
 
Mkuu ulikosea sana,tena sana.
Unanunua bajaji 5 tena kwa mkopo hiyo ni kujitafutia presha.
Hiyo moja yenyewe ukiwa nayo ni presha saa zote kuhusu usalama wa chombo,ongeza na usumbufu wa dereva.
Ilitakiwa uombe ushauri kabla hujanunua sio kuomba ushauri sasa hivi wakati maji yako shingoni.
 
Kwanza kubali kuvua uboss kwenye hii biashara .M nilianza na BM 150 2019 nilinunua kwa mtu nikampatia kijana apige kazi dgo alipiga kazi wk moja tu badae miyeyusho .. Nikaona sio noma rudi chombo angu uzuri nilikuwa najua kuendesha japo skuwa mzoefu trtb nikawa naingia nayo kazi .
Wakti natoka zangu job jion nazuga zuga road mara 10k muda mwingine 20k mpka zang sa 4 usk naenda kulala ..Nikawajiuliza jamaa anakaa na chombo 24hrs anashindwa kuleta 10k ?
Mwisho nikajisajili kijiweni na sasa nimenunua nyingine mpya kazi nafanya na boda naendesha bila wasi per day 15 had 20 skosi tena kwa muda mfupi sana..
Ukiendesha mwenyewe unalipa sana
 
Nimeona hizo pikipiki ni mkopo kutoka manispaa je kuna dhamana yoyote mliweka
Kama hakuna dhamana bas hizo pikipiki kodi za wanyonge wenzenu mtakuwa mmezifisadi maana hakuna atakayejali
Mkopo wa kukomboa vijana. Bajaj tu wanyonge ndo mlie Kam hivyo?. Sisi wenyew wanyonge ndo mana tukapata
 
Mkuu boda zliandikiwa proposal na mkopo ukatoka. Tulitk kuchenji plan tuziuze kadi zipo manispaa
 
Huo mkopo ni wa muda gani..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…