Kipondo Cha ugoko
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 878
- 1,511
Machache niyajuawayo kuhusu biashara ya barber shop.
1.hakikisha location iko vizuri(sehemu yenye movement ya watu)
2.kua mvumilivu sio umefungua biashara mwezi mmoja tu tayari Usha anza kulalamika biashara ngumu, mara hakuna wateja, saloon ni tofauti kbs na biashara nyingine kwani ukuaji wake ni taratibu. Pia mpaka watu wapate uhakika wa ubora wa huduma unayoitoa sana sana kwenye unyoaji, mtu hawezi kukurupuka tu kuja kunyoa kwako.
3.epuka kubadilisha vinyozi mara kwa mara hasa ukipata kinyoz fundi( hili zingatia)
4. Saloon iweke kiviwango sio kama genge la wahuni, utakimbiza wateja wanaojitambua na hao ndo wenye pesa nzuri .
5.usafi, aisee hapa kazia sana.pia ubora wa vifaa unavyotumia ni jambo la kuangalia sana, kama ni mashine za kunyoa nunua mashine nzuri mteja akinyoa ainjoi sio mteja aone kero. Achana na mashine za bei poa zisizo na ubora, mashine ikinyoa kichwa kimoja inachemka kama hita.
6. Kama ndo unaanza angalia zaidi kuhusu kukuza na kuipanua biashara Yako kuliko kuwa na mawazo ya kuibiwa na kinyozi, mbane kinyozi awe msafi, atoe huduma nzuri, care kwa wateja, usafi wa ofsi, awe msikivu kwa wateja n.k
7. Mwamini kinyozi wako.
8. Hakikisha unapata kinyozi/ vinyozi mafundi kweli kweli sio vinyozi wa kujifunzia kwenye vichwa vya wateja, itakula kwako.
9.kuhusu hesabu, kuwa mtu wa kufuatilia sana hiyo biashara na ushauri ni kwamba mpangie hesabu kinyozi wako akupe kwa wiki baada ya wewe kuusoma mchezo inavyoenda. Usikubali kabisa kugawana na kinyozi kinachopatikana utaumia, we mpangie hesabu then endelea na maisha mengine ya utafutaji wa maisha. Anyway Nimecheka ku- type lkn yapo mengi ya kuzingatia