Naomba ushauri kuhusu biashara ya vyuma chakavu

Abdu Amrani

Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
22
Reaction score
16
Hello brothers and sisters. Poleni na harakati wapambanani wenzangu. Niwashukuru kwa msaada tunaopeana kwenye upambanaji.

Naitwa Abdul ni mwanafunzi niko NIT nimekuwa najihusisha na biashara ya nguo tangu nianze chuo kwakushirikiana na mshikaji wangu mmoja ambae yeye yuko UDOM anamaliza mwaka huu.

Lengo la kuja kwenu ni kwamba biashara yetu ya nguo ilikufa mwaka jana,nasema ilikufa kwa sababu tuliiacha kutokana na changamoto tulizopitia (changamoto kuu ni kukosa uaminifu kwa tuliowapa usimamizi hivyo tuliamua kuacha hadi wenyewe tutakapokuwa na nafasi)

Lakini sasa mshikaji wangu anamaliza na tulishauriana turudie biashara yetu ya mwanzo ingawa kwa sasa itabidi tuanze upya kutafta wateja lakini pia hata ile frem ya mwanzo tulisharudisha na hatuipati tena.

Wakati tunawaza kuhusu hilo akatokea moja katika anko wangu ambae ye anajihusisha na biashara za kununua na kuuza vyuma chakavu na siso. Amenishawishi sana kuhusu hii biashara ingawa naogopa kuingia kwakukurupuka, nakhofia kuingia tu kwakuwa nmeshauriwa na mtu ninaemjua? Hivyo naomba kwenu wakuu yeyoye anayeelewa kuhusu hii biashara au biashara ya chupa anipe ufafanuzi zaidi tafadhali?

Ahsante. Najibu comments.
 
Hiyo biashara sio mbaya ila ujue tu, sehemu sahihi ya kuuza baada ya kununua kutoka kwa wauzaji wadogo japo najua Chimbo lipo gerezani Kariakoo.
 
Hyo biashara sio mbaya ila ujue tu,sehemu sahihi ya kuuza baada ya kununua kutoka kwa wauzaji wadogo japo najua Chimbo lipo gerezani kariakoo.
Kuna chimbo jengine pale temeke.
Huyu jamaa ndo anauziaga pale
 
Bro ingia ukiwa tayri umehitimu kabisa shule ukiwa n full time.

Nasema hv kwa kumuona kijana mmoja anampiga boss wake kwa kununua kisha anauza tena fasta kuna vyuma huu avikai kabisa stoo.

Boss akija anakuta PESA yako ipo na mzigo ulio nunuliwa pia upo kwa KG. Na balance ipo kamili.

Yapo mengi yakuandika naona uvivu.
Ukiwa n full time Hii bznes inakutoa umasikini. Usije Fanya kwa simu kabisa utatajilisha watu.
 
tatizo la chuma chakavu ni upatikanaji wake soko liko wazi sana
 
kuwa makini biashara hii na polisi ni mguu na njia yaan kukutana na kesi ni kinusa wazee wa kupita vyombo vya moto machimbo yao ni hayo
 
Much respect bro sem nn nilitaman tuongee zaid kaka
 
Una mtaji WA kiasi gani.??? Mimezaliwa kwenye biashara hii japo kwa sasa siifanyi ila naijua nje ndani.
 
kuwa makini biashara hii na polisi ni mguu na njia yaan kukutana na kesi ni kinusa wazee wa kupita vyombo vya moto machimbo yao ni hayo

Kuna friend wangu aliingia king baada ya aliyekua partner wake kumzunguka, mzigo wenyewe ulikua wa wizi asee, zilimtoka hela balaa chini ya corrupted polisi, jamaa hana hamu tena na hiyo biashara.
 
Asante kwa ushauri kaka
Kuna mtu alikamatwa anangoa misalaba ya chuma , anauza chuma chakavu, alikamatwa na alikuwa lumande, wengine watoto wanaiba machuma kwao, wazazi wakifatilia wakivikuta kwao msala huo, haya yametoa kwenye jamii zetu.
 
Kuna mtu alikamatwa anangoa misalaba ya chuma , anauza chuma chakavu, alikamatwa na alikuwa lumande, wengine watoto wanaiba machuma kwao, wazazi wakifatilia wakivikuta kwao msala huo, haya yametoa kwenye jamii zetu.
Sahihi changamoto ndo maisha
 
Kuna friend wangu aliingia king baada ya aliyekua partner wake kumzunguka,mzigo wenyewe ulikua wa wizi asee,zilimtoka hela balaa chini ya corrupted polisi,jamaa hana hamu tena na hiyo biashara.
Duuuu halo sema ndo biashara mapambano
 
hiyo biashara inalipa sana lakini upate sehemu angalau kwa mwezi utoe tani 10 uwezi kosa faida ya m 1 ngoma sehemu ya kujazia mzigo huo kwa mwezi
Tani moja ya chuma ni laki6, tan ya aluminium ni zaidi ya mil1 nafikiri ni kama mil1.2 cha muhimu kwenye hiyo biashara ni connection ya kupata mzigo na pa kuuzia baasi kuna watu wanateka hata magari wanakata kata....kunao wanaingia humo zambia viwandani, mavyuma ya tanesco ukiwa na connection, ni biashara nzuri inayohitaji pia kukaza roho
 
Kuna mtu alikamatwa anangoa misalaba ya chuma , anauza chuma chakavu, alikamatwa na alikuwa lumande, wengine watoto wanaiba machuma kwao, wazazi wakifatilia wakivikuta kwao msala huo, haya yametoa kwenye jamii zetu.
Akishakuwa kibiashara hizo za nyumbani vinakuwa tu vya kudanganyishia, wafanyabiashara ambao tayari washatengeneza connection hasa kwenye kamati za ulinzi za mkoa ujue ni kama tu majambazi yaan ni biashara haramu kutokana na upatikanaji wa malighafi kunao wanang'oa transformers vyuma vya reli, viwandani humo, ofcoz wanapiga pesa ila dah....nasema hivo sio kama nimesimliwa
 
Kweli kabisa, wamisalaba alikuwa anangoa makaburi ya kola Moro, walipozika wale walioungua ajari ya lori la mafuta, alitangazwa mpaka kwenye vyombo vya habari.
 
Tafuta biashaea nyingine, bado u mdogo, ujaoa, una elimu kwa nini ufanye biashaea ya risk hivi? Haifai kabisa, kila unapoletea bidhaa ujue ni mwanzo wa kwenda lock up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…