Naomba ushauri kuhusu Bima za Magari

Naomba ushauri kuhusu Bima za Magari

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Habari wakuu.

Naomba msaada wa mawazo kuhusu kununua bima ya gari. Nilikua nataka kukata comprehensive, ila kuna mdau akaniambia badala ya kwenda kwa ofisi za bima moja kwa moja ni bora kupitia kwa agent.

Mdau akasema ukipata shida ni rahisi kulipwa km ulikata kwa agent maana process atafuatilia yeye zote kuliko kwenda ofisini maana mlolongo unakua mrefu. Agent hulipwa kamisheni ndio maana hupambana ili wapate wateja wengi.

Hii ikoje kwa wazoefu wa haya mambo walioko humu?

Anyway, gari liko mkoani sio Dar

Asanteni sana
 
Siku ukipata shida agent hana cha kukusaidia zaidi ya kukuelekeza ofisi ilipo
 
mimi nilikatia bank ya NMB nafikiri wao watamaliza kila kitu ili kutochafua sifa ya benki yao.
 
Maagent kwa sasa wana kazi, maana Mabenki na Simu zote zakata BIMA
 
Maagent kwa sasa wana kazi, maana Mabenki na Simu zote zakata BIMA
Mdau aliniambia maanget wanapambania kiasi kwamba mteja akipata shida wao mdo wanafuatilia kila kitu ili kuondoa usumbufu kwa mteja na kuvutia wateja wengi
 
Mdau aliniambia maanget wanapambania kiasi kwamba mteja akipata shida wao mdo wanafuatilia kila kitu ili kuondoa usumbufu kwa mteja na kuvutia wateja wengi
Kampuni itakuwepo daima lakini mwanadamu hana garantii.
Nenda ofisini.
Comprehensive ni pesa ndefu utachezewa mchezo mchafu.
 
Mimi nipo benki flani hivi, kuhusu ukataji bima wetu sisi tupo tofauti sana ukija kwetu tunakukabidhi staff atakaekushughulikia issue yako mwanzo mwisho. Ukipata majanga we unampigia tu then yeye ndo anafuatilia kila kitu mpaka kuhakikisha kitu kinaisha. Ili kufanikisha hilo tunakuwa na ushirikiano na makampuni ya bima kwenye wafanyakazi. Mfano labda tumeingia ubia na jubilee basi tunachofanya jubilee wanachukua staff wao wanamleta kwenye benki yetu ambapo pia na sisi tunampa mkataba kama mfanyakazi wetu, sasa kule kwenye bima watamlipa mshahara sisi tunampa commission. Hii inasaidia ikitokea shida kwa mteja inasolvika haraka maana huyu anayekuhudumia anafahamika kote
 
Back
Top Bottom