Naomba ushauri kuhusu Deep Poll na cheti cha kifo

Naomba ushauri kuhusu Deep Poll na cheti cha kifo

She is Aisha

New Member
Joined
Jun 1, 2024
Posts
4
Reaction score
2
Habari ZENU,

Mimi nilivyomaliza shule ya Msingi nilipelekwa Lushoto, huko sikusoma form one ilikuwa direct form two na kaka angu mtoto wa ba mkubwa ndie alikuwa ananisimamia kusema nina akili nisisome form one.

Baadae akaniambia jina langu limegoma hivyo akaniandikia jina la mdogo wake ambae tunafanana jina la mwanzo, Kaka angu tulikorofishana, Mwaka huu mwanzoni baba angu alifariki sasa nataka kwenda chuo.

Bado sina cheti cha kuzaliwa. Nilihitaji kuaattach cheti cha kifo cha baba ili iwe rahisi kupata mkopo lakini jina la kitaaluma tofauti na la baba naombeni ushauri wenu jamani🙏 Wasijesema nimeghushi.

Pia nimeshauriwa kuhusu deed poll je itawezekana kwenye kupata mkopo?!
 
Wewe ushajichanganya hapo kwenye kutokusoma form 1, kwa yaliyotokea mlaumu kaka yako japo haitasaidia kitu pengine ni kutokujua ila hapo kwa mfumo wa sasa itakusumbua sana kupata mkopo ila pambana
Pole sana na sir god akutie nguvu
 
Mbona umempa jibu la kifedhuli sana. Jaribu kuwa na utu, si lazima uchangie kila uzi mkuu. Nilifikiri una hekima kumbe ni wale wale wajuaji tu
Wapi umeona nimechangia kila uzi? Wapi nimeleta ufedhuli! Haya lini tulishawahi kuongea nikakwambia nina busara?
Nilitarajia ungetoa mchango wako unaohusiana na uzi badala yake umekuja kunishambulia?
 
Wapi umeona nimechangia kila uzi? Wapi nimeleta ufedhuli!
Nilitarajia ungetoa mchango wako unaohusiana na uzi badala yake umekuja kunishambulia?
Ulichojibu kinaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye very low EQ
 
Ulichojibu kinaonyesha kuwa wewe ni mtu mwenye very low EQ
EQ ❎❎❎
IQ✅✅✅

Pamoja sana ndugu leonardo da vinci una akili nyingi sana kuliko members wote humu jf
 
EQ ❎❎❎
IQ✅✅✅

Pamoja sana ndugu leonardo da vinci
Yaani umejipa hadi u Dr. na hujui kuwa EQ inamaanisha Emotional quotent na si IQ (Intelligency Quotent). Nimethibitisha ulivyo mwepesi sana upstair na inawezekana hata IQ pia iko chini sana. Punguza ujuaji mkuu.
 
Stick kwenye mada sijaona coment yoyote ulotoa yenye kumsaidia mtoa mada zaidi ya kuona wenzio hawana akili hii ni jf kila mtu anachangia anavyoona hizo EQ unazoleta hapa ni janja janja tu
 
Stick kwenye mada sijaona comentbyoyote ulotoa yenye kumsaidia mtoa mada zaidi ya kuona wenzio hawana akili
Ungefuta kwanza komenti yako iliyojaa ubinafsi na ujuaji. Wapo wajuvi na wenye utu watamsaidia tu.
 
Yaani umejipa hadi u Dr. na hujui kuwa EQ inamaanisha Emotional quotent na si IQ (Intelligency Quotent). Nimethibitisha ulivyo mwepesi sana upstair na inawezekana hata IQ pia iko chini sana. Punguza ujuaji mkuu.
Ndio shida ya jf kwa vile umeona id ni jina la kike unataka kujikosha kosha ili akuone una huruma uzame pm kiurahisi😀😀
 
Ungefuta kwanza komenti yako iliyojaa ubinafsi na ujuaji. Wapo wajuvi na wenye utu watamsaidia tu.
Hii comment ingekua mbaya mods wangefuta na ningekua banned mkuu..
Kufuta comment sio kazi yangu.

OVA
 
Jamanii naombeni samahanii kiukweli nahitaji ushauri wenu sana hizo mis understanding sio nzuri, samahanini yaanii mm nahitaji ushauri nisaidieni tu hata sielewi wakuu🙏 Nasubiria majibu yenu.
 
Kwa jinsi tatizo lilivo ni ngumu kusolve, hapo nakushauri chukua cheti cha kifo nenda nacho Rita tafuta mtu atakayekupa muda wa kukuzikiliza shida yako kwa undani zaidi na umuombe akusaidie kubadikisha jina la mzee lifanane na lako ila kumbuka kabla ya yote mtafuta huyo bro aliyekuleta shida akutafutia kama kilo moja uwe nayo mkononi then nenda Rita utasaidiwa. Kwa ufupi kwa situation ilivyo hapo ni rahisi zaidi marehemu baba kufuata majina yako yaliyokosewa kuliko wewe kufuata majina majina sahihi ya baba.
 
Back
Top Bottom