Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Mazda Atenza 2015

Wadau samahani tena nauliza kuna utofauti kati ya mazda atenza na mazda 6 mana naona beforward wamezitofautisha
Kama walivyosema wazee, zote ni gari moja tofauti ndogo sana.

Mazda 6 iliuzwa nje ya Japan kwahiyo kwingine kwote Duniani iliitwa Mazda 6 kasoro Japan ikawa Mazda Atenza.

Mfano mwingine ni Mazda 3 kwote Duniani iliuzwa ivyo ila Japan ikawa Axela.

Huu mchezo Japan kawaida yao ata Toyota IST (Scion xA), Altezza (Lexus IS 200), etc.

Turudi kwenye topic; pamoja na yote tofauti zipo kidogo, mfano:

1. Mazda 6 za nyuma ya ,2015 zina knob ya kucontrol infotainment.

2. Mazda 6 zina options ya Petrol mostly.

3. Upholstery nzuri kwenye Mazda 6.

4. Mazda 6 zina Sport Mode.

5. Mazda 6 zina ushuru mkubwa balaa.

Ila mwisho wa yote, NO SINGAPORE.
 
Unainjoi sana! Skyactiv tech ni super quiet, angalia sana watu wa petrol station wasije kukuwekea petroli badala ya diesel!! Wahudumu huwa wanakariri gari ndogo zote ni za petroli.
Yeah nipo makini mzee. Hafu Puma waliniwekea kastika ka Diesel kwa ndani. Napenda kuweka Puma & Total. Kwingine by emergency.
 
Hii gari inataka clean Diesel popote utakapoweza kuipata
Clean diesel bado hatuna hii gari nataka ultra low Sulphur diesel! kitu ambacho hakipo hapa kwetu ! Eventually ukiwa na hii gari baada ya Muda itakulazimu kufanya dpf deletion, maana Sulphur ya diesel yetu italifanya dpf kuziba mapema kuliko ambayo lingetumia ultra low Sulphur diesel.
PUMA Orxy na Total wana mafuta mazuri ila bado Sulphur content ni kubwa.
 
Delete niliona expensive, jamaa alisema 800k mwingine 1.2m nikaona bora nisubiri Kenya rally ijayo niende wakanifutie wao walisema kwa 350k Tsh.
 
Delete niliona expensive, jamaa alisema 800k mwingine 1.2m nikaona bora nisubiri Kenya rally ijayo niende wakanifutie wao walisema kwa 350k Tsh.
Kenya wapo advanced sana, diesel deletion ni software issue, then itabidi manually uliondoe Hilo muffler kind of a thing( dpf)
Mazda ni gari pekee ndogo inayouzwa huko japan ikiwa na diesel engine ambayo ni very advanced na kwa bei poa kabisa.
Tra wanataka kuharibu show ya hii gari kwa mikodi yao iso na kichwa wala miguu.
 
Lazima watazidi kuongeza tu. Wakiona gari imependwa wanazidisha kodi.
 

Wanaanza kutoboa ndo wanafanya DPF delete. Hiyo ya kuiprogram ECU sasa ndo watu wanaringa nayo. Ila nadhani wanafanya tu expensive bila sababu. Labda zotashuka watu wakiwa nazo
 
N
Ni AWD,RWD au 2WD?
 
Iyo handbrake ndio sababu kubwa kukimbia 2014 mkuu, kama bei hazitopishana sana ntachuku 2016
Bila shaka ww sio mtu wa Magari sana..

Ikiwa mtu wa magari hasa..

Option ya kwanza ni hiyo handbrake ikae mkao like that, number mbili gari iwe MANUAL.

hizi Option zote kwako ni batili..

So far so good kimfaacho mtu chake!!!
 
Bila shaka ww sio mtu wa Magari sana..

Ikiwa mtu wa magari hasa..

Option ya kwanza ni hiyo handbrake ikae mkao like that, number mbili gari iwe MANUAL.

hizi Option zote kwako ni batili..

So far so good kimfaacho mtu chake!!!
Handbrake ikae hivyo ili isaidie Nini?Au video za ku-drift zinakudanganya mzee?
 
Front Wheel Drive.

Nadhani hawajawahi toa RWD na AWD ndio maana US wengi wanaziponda (sijui kwasababu ya Winter kwao).
Dahh nishabadir mawazo.. ila kwa matumiz tu ya kawaida ni nzr.. sana sana.

Naona kwa mafuta/Mileage tunaweza fananisha na Premio.. right?

I prefer RWD with Manual Transmission..
 
Wadau hivi kwanini gari za Singapore is a no go zone?
Sababu nyingi ila kuu "nnayosikia" annual car inspection yao sio makini sana kama ya JP.

Iko hivi; magari yenye umri zaidi ya 10 years kwao yanahitaji inspection kila mwaka, magari yenye miaka 3 hadi 10 yenyewe kila baada ya miaka miwili.

Sasa "nnavosikia" ukaguzi wao haupo serious sana ni kama sisi kila mwaka unavoenda kwa traffic officer unampa elfu 7 anakupa stika ya nenda kwa usalama.

Pia, kurudisha odometer nyuma Singapore sio kosa kisheria. Kwahiyo mtu anaweza rudisha kutoka 100k hadi 40k na fresh tu.


Na vingine wataongezea
 
Dahh nishabadir mawazo.. ila kwa matumiz tu ya kawaida ni nzr.. sana sana.

Naona kwa mafuta/Mileage tunaweza fananisha na Premio.. right?

I prefer RWD with Manual Transmission..
RWD tena manual sedan au yoyote? Maana kama sedan hapo naona kabisa dalili za kwenda Ujerumani.
 
RWD tena manual sedan au yoyote? Maana kama sedan hapo naona kabisa dalili za kwenda Ujerumani.
Sedan..

Mbona zipo nyingi tu.. kwa mjapenga, mfano Aristo's, Mazda zipo hasa Rx7/8, Altezza.. etc etc.. the problem is.. kupatq yenye ultra specs kama hizo za Atenza ni ngumu sana.. mfano hiyo fuel consumption aisee nimeipenda. Ktk hizo gari za Mjapan hasa Toyota ni kichefuchefu.

Mfn Aristo uipate yenye 2jzGte au 2JZ kavu (N/A) si chini ya CC 3k-3.5k.. ambayo itakup mileage ya 5/6 per Lt. Wakat ww mwenye Atenza unaenda 13-15/lt.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…