Naomba ushauri kuhusu gari aina ya Mazda Atenza 2015

Wanaanza kutoboa ndo wanafanya DPF delete. Hiyo ya kuiprogram ECU sasa ndo watu wanaringa nayo. Ila nadhani wanafanya tu expensive bila sababu. Labda zotashuka watu wakiwa nazo
Kutoboa dpf kunasababisha check engine code na ecu italiweka gari kwenye limp home mode na kusababisha torque reduction by 70% .ni kama tu vile adblue inavyorusha code ikiisha kwenye reserve tank.
Best practise ni kufanya dpf delete then unatoboa au kuliondoa kabisa hilo dubwana. Gjarama za kufanya kwetu ni kubwa kwa sababu mafundi wetu wengi ni vilaza wachache wanaojua ndo hao wanaringa na mibei ya juu
 
Altezza naona kama old sana. Angalau IS 300 ile nadhani ni RWD.
 
Gharama za kufanya kwetu ni kubwa kwa sababu mafundi wetu wengi ni vilaza wachache wanaojua ndo hao wanaringa na mibei ya juu
Hapa kwenye bei hapo.. Kali sana.
 
Altezza naona kama old sana. Angalau IS 300 ile nadhani ni RWD.
Yeah but inapokea mods vzr sana....

Nimeona Atenza zipo Manual pia. Ubaya nyingi ni left hand.. (UK versio) gari iwe Manual alaf Left hand aisee
 
Bila shaka ww sio mtu wa Magari sana..

Ikiwa mtu wa magari hasa..

Option ya kwanza ni hiyo handbrake ikae mkao like that, number mbili gari iwe MANUAL.

hizi Option zote kwako ni batili..

So far so good kimfaacho mtu chake!!!
Kwa sasa natumia lexus is200 mkuu ina iyo handbrake ya kuvuta sasa nataka kutest new technology niachane na mikweche ya kizamani
 
Yeah but inapokea mods vzr sana....

Nimeona Atenza zipo Manual pia. Ubaya nyingi ni left hand.. (UK versio) gari iwe Manual alaf Left hand aisee

Hakuna UK version left hand, hizo itakuwa version za marekani, Canada, au nchi nyingine za Ulaya na Asia. UK wanapenda manual ila ni RHD. Na marekani na Canada na baadhi ya nchi za Ulaya wanaziita Mazda 6
 
Yeah but inapokea mods vzr sana....

Nimeona Atenza zipo Manual pia. Ubaya nyingi ni left hand.. (UK versio) gari iwe Manual alaf Left hand aisee
UK na Ireland wanatumia right hand vehicles, left hand zipo Belgium Netherland Denmark n. K
Gari za manual zimepitwa na wakati na kwa mafoleni haya ya Tz utakuwa unajitesa tu.
 
Mkuu assante sana natunai umenipa nguvu ya kuchukua hii chuma naona nichukue model ya 2015 assante pia natumai hii kitu itakuwa na comfort nzuri tu
Kaka upo ubungo ipi hii chuma naielewa sana ila nakuwa muoga kwasababu siijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…