Naomba ushauri kuhusu hii biashara ya mashine ya miwa

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,042
Reaction score
2,005
Habari ndugu zangu, kuna jamaa yangu ameniomba nimfungulie mashine ya miwa jijini Dar, akasema atakuwa ananipa sh 15,000/=kwa siku.

Sasa ndugu zangu mnisaidie kujua gharama ya kila kitu na je sio kwamba atakuwa ananipiga? Make mimi sijawahi kufanya hiyo biashara. Mwenye uzoefu anisaidie jamani nione eitha nifungue au niache hasa kwa kuangalia maslahi.

Tusaidiane jamani make mimi nipo Tanga huko sasa mkinipa mchanganuo nitawashukuru sana. Naomba kujua bei za mashine, materials na vitu vingne.
 
Ngoja wadau wenye uzoefu waje...
 
Mfanyie hata elfu 10 umkwamue kwenye ukata ukisha jilipa muachie
 
Biashara ni location, hivyo ni ngumu Mtu kutoa ushauri wa jumla ili hali kuna sehemu akiwepo anaweza ale za uso na kuna mahali akitegesha hata hiyo itakuwa ndogo.

Ni yeye ndio akupe maelezo ni wapi anapalenga kuweka hiyo biashara na akupe uzoefu wake kwenye hiyo kazi...then kuanzia hapo waweza kufanya utafiti wako binafsi kujua kama kweli eneo tajwa linaweza kulipa.

Mashine zina bei tofauti kutegemea na wapi unanunulia, kama ni mpya au used n.k., ni kuanzia laki sita mpaka milioni na nusu hivi.
 
Me nafanya hyo biashara ila ni mkoan ngoja tuwasubiri wadaslama waje kutoa michango yao
 
Me nafanya hyo biashara ila ni mkoan ngoja tuwasubiri wadaslama waje kutoa michango yao
Yafaa utoe udhoefu wako wa huko mkoani ili aweze kuunganisha dot mwenyewe mkuu.
 
Sahihi mkuuu ,angeweza kunitoa matongotongo aiseee
Mkuu we mfungulie hiyo 15 inawezekana japo itategemeana na location kuhus bei za mashine inategemeana zipo kuanzia laki 8 had Milion na 20 kuna za umeme na jenereta pia zipo za mkono na mzgo mmoja wa miwa kwa dar inakaa miwa 20 me nanunua kwa elf 11 mzg mmoja ambao muwa mmoja unaweza kutoa gras mbili za moto ambazo moja tunauzaga elf 1 na za bard anaweza kutoa 4 had 3 sasa kama anaweza kumaliza mzgo mmoja kwa siku anaibuka hata na 30k atatoa garama ya tangawiz na ndimu labd na usafir na mabaraf ni kama 5k huo ni mzg mmoja wa miwa 20 kama atauza zaid ya hapo mtaelewana, risk muda mwingn anaweza kupata mzgo wenye miwa miembamba san au mikavu so kiwango kitapungua la kumalizia juic ya miwa kam unatak kulaza basi ilalrle kweny friji
mchawi wa mafanikio ni usafi tu
Nawasilisha πŸ™πŸ™
 
Mkuuu nakushukiru kwa kunifungua macho
 
Location jamani wapi hizo mashine zinapatikana, je Mwanza zipo?
 
Location jamani wapi hizo mashine zinapatikana, je Mwanza zipo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…