Naomba ushauri kuhusu hii kesi

Dodo86

Member
Joined
Oct 23, 2018
Posts
99
Reaction score
83
Hivi file linaweza likapotea mahakamani na kama halionekani hatua gani inafata?

Kwa kifupi Mama yangu alikua ana kesi yake ya nyumba takriban imeenda miaka Tisa na mwaka jana mwezi wa tisa alishinda kesi na tukaanza process ya kukaza hukumu mara tena ghafla kila tukienda mahakamani tunaambiwa file halionekani kwahiyo tukawa tunapigwa calender tu na mpaka mawakili wake wakadraft barua mahakamani kulalamika lakini hamna kilichofanyika.

Wiki iliopita tuliambiwa turudi Leo tarehe 12.08.22 still bado file halikuonekana na hakimu amesema ijumaa turudi tena kama halijaonekana kikao kitafanyika kuhusi hili swala.

Nina maswali mawili kwanza: File linaweza kupotea mahakamani?

Pili: Na kama halijaonekana unaweza kutumia copies maana mawakili wa mama copies wanazo.

Naombeni ushauri kwa wanaojua mambo haya.

Ahsanteni.
 
Halijapotea, limefichwa mpaka utoe hela...
Ndio maisha ya kibongobongo...pole sana
 
Ni mahakama ngazi gani? Mwanzo, wilaya, au mahakama kuu? Tufahamu kwanza hilo
 
Halijapotea, limefichwa mpaka utoe hela...
Ndio maisha ya kibongobongo...pole sana
Tumeshawapa makarani kama wawili hela ila hamna kitu kila ukienda wanakupiga calender na wanakwambia watakupigia simu
 
Tumeshawapa makarani kama wawili hela ila hamna kitu kila ukienda wanakupiga calender na wanakwambia watakupigia simu
Mshindani wako anamwaga mpunga mwingi kuliko wwe, ndiyo maana una soundishwa na file lako! Kesi siku hizi ni biashara ndiyo maana mtu akiwa na hela tu haogopi hata kuwa, maana anajua waamuzi wa hizo kesi wako komaslahi zaidi na siyo kweli kwa kuangalia haki! Lakini usife Moyo pambana Mungu atakuongoza na utakutana na wapenda haki wa ukweli na watakusaidia kweli bila hata ya kutoa shiling yako mfukoni!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…