Naomba ushauri kuhusu hili tatizo la macho

Teamanaconda

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2013
Posts
602
Reaction score
564
Habari wanajukwaa,

Nina mama yangu ameanza kupata tatizo la macho tangu juzi, tulimpeleka hospital wakasema macho yameanza kuweka mtoto na anapresha ya macho.

Hivyo tumeshauriwa tumnunulie miwani, je kuna yoyote humu ambae ameshawahi kukutana na tatizo hili,na je uliweza kulitibu kwa njia gani? Mama yangu kwa umri yupo 60.

Nawasilisha
 
Pressure ya macho (macular degeneration) na mtoto wa macho (cataract) ni vitu viwili tofauti. Muone eye surgeon mzuri akupe ushauri.
Presha ya macho ilikuwa imenianza. Jicho la kushoto liliingiliwa na kakitu kadogo sana likawa linauma uma nakuwa uncomfortable. Kumbe kale ka foreign body kamekuwa embedded kwenye cornea. Nimekwenda kwa optometrist kwa observation ya kawaida kupiga picha huyoo akapaniki akadhani ni kansa kwa sababu kale ka foreign body kalikuwa kamejenga mishipa yake ya damu.

Nilipoenda kwa mtaalamu ndo nikaambiwa presha pia ilikuwa juu sana hasa hilo jicho la kushoto lenye matatizo. Aliweza kukatoa hako ka foreign body (vimbegu hivi vidogo sana vyenye mabawa vinavyorushwa na upepo) na bahati nzuri cornea ilikuwa haijaathirika. Na retina na maeneo mengine muhimu yalikuwa sawa.

Ili kuishusha presha ya macho nilipigwa laser session tatu na presha ikaweza kushuka kutoka 33 mpaka sasa 21 ambayo ni ya kawaida. Hata ile mishipa ya damu iliyokuwa imetokea ili kukalisha hako ka foreign body nayo imekufa japo mingine bado ipo. Mtaalamu kasema atakuwa anaiangalia kila baada ya miaka miwili na nikihisi tu maumivu katika hilo jicho nimwambie mara moja.

Kumbe ningezubaa ningeingia kwenye matatizo makubwa na hata upofu huko mbele ya safari.

Mungu ni mwema na huyo ndugu ampeleke mama kwa specialist mzuri watamsaidia. Ila sidhani kama presha ya macho inaweza kutatuliwa kwa kuvaa miwani. Kuna dawa ya maji (eye drops) anaweza kupewa akawa anatumia au hiyo tiba ya mionzi (laser) kama niliyofanyiwa mimi. Cataract (mtoto wa jicho) pia wanaweza kufanya operesheni na kuiondoa.
 
Kuna surgery inaitwa LASKI unapona kabsa macho nawewe ulizia kwa bongo kama ipo na Bei yake
 
Mungu ni mwema na huyo ndugu aende tu kwa specialist mzuri watamsaidia.
Hospital gan iyo?? Unaweza kunipatia namba za specialist yoyote wa macho
 
Bahati mbaya sikutibiwa Tanzania mkuu. Kwa Tanzania sijui hata ni hospitali gani ndugu yangu. Wenye habari zaidi watakuja kukusaidia. Mama atapona tu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Pressure ya macho (macular degeneration) na mtoto wa macho (cataract) ni vitu viwili tofauti. Muone eye surgeon mzuri akupe ushauri.
Nina myopia ya juu navaa -6.5 Kwa -7.0...age below 30

Kuna kipindi nilianza kupata hiyo increase in occular hypertension wenyewe wanasema kwenye jicho moja nikaanza kutumia dawa imeacha. Pia last time nilipima nikaambiwa jicho limeongezeka size to the last point sijui ya 26mm

Ushauri tafadhali wa nini nifanye walau kuendelea kuyalinda macho yangu yasiendelee kwenda kuwa worse Zaid..🙏
 
Huko huko ulikopata tiba uwe unafanyiwa review angalau mara moja kwa mwaka.
 
Kuna surgery inaitwa LASKI unapona kabsa macho nawewe ulizia kwa bongo kama ipo na Bei yake
Lasik surgery ni ya kusaidia uonaji tu hasa kama unavaa miwani au unatumia contact lenses. Inakurudisha kwenye uoni timilifu wa 20/20 lakini haisaidii matatizo mengine. Na ukiwa na ishu zingine (cataracts, glaucoma...) wala hawakufanyii. Na gharama yake si mchezo. Ndo maana wengi tunavaa tu miwani!

Screenshot_20220203-143107_Chrome.jpg
 
Habari wanajukwaa,nina mama yangu ameanza kupata tatizo la macho tangu juzi,tulimpeleka hospital wakasema macho yameanza kuweka mtoto na anapresha ya macho,hivyo tumeshauriwa tumnunulie miwani,je kuna yoyote humu ambae ameshawahi kukutana na tatizo hili,na je uliweza kulitibu kwa njia gani?.Mama yangu kwa umri yupo 60+.nawasilisha
Mkuu Maradhi ya presha ya macho (Glaukoma) na Maradhi ya mtoto wa jicho aka Cataract Ni Maradhi 2 Tofauti kabisa.Ushauri mpeleke kwa Mtaalam wa maradhi ya macho akampime na kusema mama yako anayo maradhi gani?

ili tuweze kumtibia maradhi yake. Na Asitumie miwani ya macho kwani haitoweza kumsaidia kitu kama ana maradhi ya presha ya macho au maradhi ya mtoto wa jicho pia miwani haitoweza kumsaidia kitu huyo daktari aliye kwambia mama yako atumie miwani ni dakaari hajuwi kitu .Mtafute Daktari mzuri ili aweze kumpima mama yako vizuri.

Kisha ulete mrejesho wako hapa mama yako ameambiajwe na Daktari kuhusu maradhi yake ya macho? Kisha ukitaka atibiwe kwa dawa zetu za asili atatibiwa na kupona pasipo na kutumia miwani ya macho auguwe pole mama yako.

Mkuu Maradhi ya presha ya macho (Glaukoma) na Maradhi ya mtoto wa jicho aka Cataract Ni Maradhi 2 Tofauti kabisa.Ushauri mpeleke kwa Mtaalam wa maradhi ya macho akampime na kusema mama yako anayo maradhi gani? ili tuweze kumtibia maradhi yake. Na Asitumie miwani ya macho kwani haitoweza kumsaidia kitu kama ana maradhi ya presha ya macho au maradhi ya mtoto wa jicho pia miwani haitoweza kumsaidia kitu huyo daktari aliye kwambia mama yako atumie miwani ni dakaari hajuwi kitu .Mtafute Daktari mzuri ili aweze kumpima mama yako vizuri. Kisha ulete mrejesho wako hapa mama yako ameambiajwe na Daktari kuhusu maradhi yake ya macho? Kisha ukitaka atibiwe kwa dawa zetu za asili atatibiwa na kupona pasipo na kutumia miwani ya macho auguwe pole mama yako.

Asante sana mkuu kwa ushauri wako,alafu kingine kilichoniacha hoi,yani Dr anakwambia miwani ukikaa ndani ya siku tatu hujaja kununua tunamuuzia mtu mwingine,kwa elimu yangu ndogo ya UPE nikajua hapa tunataka kuuziwa miwani tu.hakuna matibabu.
 
Habari wanajukwaa,

Nina mama yangu ameanza kupata tatizo la macho tangu juzi, tulimpeleka hospital wakasema macho yameanza kuweka mtoto na anapresha ya macho.

Hivyo tumeshauriwa tumnunulie miwani, je kuna yoyote humu ambae ameshawahi kukutana na tatizo hili,na je uliweza kulitibu kwa njia gani? Mama yangu kwa umri yupo 60.

Nawasilisha
Uvutaji wa bange nasikia unaponyesha presha ya macho
 
Pressure ya macho (macular degeneration) na mtoto wa macho (cataract) ni vitu viwili tofauti. Muone eye surgeon mzuri akupe ushauri.
Gombeyehealthcare,
Tunazo huduma mahususi kwa changamoto za macho.

Na vilele Tunatoa huduma zifuatazo.
1. Matatizo ya Mifupa.
2. Matatizo ya Mmengonyo wa Chakula.
3. Matatizo ya Mfumo wa uzazi kwa jinsia zote. nk

Wasiliana nasi kwa namba.
+255 678 211 747
+255 733 482 038
Tunapatikana Dar es salaam ILALA, na mikoani kote Tunatoa huduma.
 
Pole bro
Presha ya macho ilikuwa imenianza. Jicho la kushoto liliingiliwa na kakitu kadogo sana likawa linauma uma nakuwa uncomfortable. Kumbe kale ka foreign body kamekuwa embedded kwenye cornea. Nimekwenda kwa optometrist kwa observation ya kawaida kupiga picha huyoo akapaniki akadhani ni kansa kwa sababu kale ka foreign body kalikuwa kamejenga mishipa yake ya damu.

Nilipoenda kwa mtaalamu ndo nikaambiwa presha pia ilikuwa juu sana hasa hilo jicho la kushoto lenye matatizo. Aliweza kukatoa hako ka foreign body (vimbegu hivi vidogo sana vyenye mabawa vinavyorushwa na upepo) na bahati nzuri cornea ilikuwa haijaathirika. Na retina na maeneo mengine muhimu yalikuwa sawa.

Ili kuishusha presha ya macho nilipigwa laser session tatu na presha ikaweza kushuka kutoka 33 mpaka sasa 21 ambayo ni ya kawaida. Hata ile mishipa ya damu iliyokuwa imetokea ili kukalisha hako ka foreign body nayo imekufa japo mingine bado ipo. Mtaalamu kasema atakuwa anaiangalia kila baada ya miaka miwili na nikihisi tu maumivu katika hilo jicho nimwambie mara moja.

Kumbe ningezubaa ningeingia kwenye matatizo makubwa na hata upofu huko mbele ya safari.

Mungu ni mwema na huyo ndugu ampeleke mama kwa specialist mzuri watamsaidia. Ila sidhani kama presha ya macho inaweza kutatuliwa kwa kuvaa miwani. Kuna dawa ya maji (eye drops) anaweza kupewa akawa anatumia au hiyo tiba ya mionzi (laser) kama niliyofanyiwa mimi. Cataract (mtoto wa jicho) pia wanaweza kufanya operesheni na kuiondoa.
 
Gombeyehealthcare,
Tunazo huduma mahususi kwa changamoto za macho.

Na vilele Tunatoa huduma zifuatazo.
1. Matatizo ya Mifupa.
2. Matatizo ya Mmengonyo wa Chakula.
3. Matatizo ya Mfumo wa uzazi kwa jinsia zote. nk

Wasiliana nasi kwa namba.
+255 678 211 747
+255 733 482 038
Tunapatikana Dar es salaam ILALA, na mikoani kote Tunatoa huduma.
mpo ilala ipi
 
Back
Top Bottom