Naomba ushauri kuhusu kiwanda cha vinywaji

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
Habari za mchana huu!! Katika harakati za kutafuta maisha nimepata wazo la kufungua kiwanda cha vinywaji yaani Juice,soda katika taste tofauti tofauti... Kuhusu pesa ninazo (ila si za kuhonga madem) sasa nataka munisaidie A to Z ili niweze kukamilisha Jambo hili... Nakaribisha ushauri na changamoto zake. Tanzania ya viwanda ndo hii wajamen
 
Aisee hili wazo ni kubwa saana, Nadhani tafuta manufacturing business consultants au zama kisiri kwenye viwanda ulivyotaja ukiwa kama kibarua, hii itakusaidia kujua 2,3 ya uendeshaji wa viwanda hivi. Hapa Utapata ushauri ila sidhani Kama utakidhi mahitaji
 

Kama huko tayari wasiliana na mimi kwny namba 0715058481
 
Endelea kutafuta maisha bhana
 
Aiseee ungemuambia kwa nini aanze na maji.
Maji hayana complications nyingi kwenye utengenezaji wake ukilinganisha na juice ambazo zinahitaji blending mixtures ya vitu vingi.
Lakini kwenye maji ukishachimba kisima kinachofuata ni kuwa na mashine za Disinfectant/filters kwa ajili ya kuyasafisha tu.
Then baada ya hapo unayapakia na kuyapeleka sokoni kwa hiyo maji huwa hayana hasara.
Kitu kingine pia maji huwa hayaharibiki unapoyahifadhi kwenye tanks kwa muda mrefu lkn kwa upande wa soda au juice usipoipakia kwa wakati kwenye chupa zake huwa zinaharibika na hvyo kupata hasara za mara kwa mara endapo soko lako halijatengamaa vizuri.
Kwa ushauri zaidi upande wa Engineering/Installation of Beverages machines mnakaribishwa inbox.
 
Reactions: amu
Na pia ukiacha kiwanda Cha maji kiwanda kingine ambacho ni mbadala wa kiwanda Cha maji ni kiwanda Cha Spirits/Whisky/Brandy na process zake zinafanana sana na maji ila zinatofautiana kwa kiasi kidogo sana.
Na pia ukija kwenye upande wa mauzo bado zina soko zuri sana yaani hazina ushindani mkubwa Kama ilivyo ktk soda,juice na maji.
Hadi hii leo viwanda ambavyo vimekamata soko la nchi nzima ni Konyagi na Kvant tu.
KampuniZingine zilizobaki zimekamata masoko ya kimkoa tu na kanda.
Ingawa sijajua imani yako ipoje lkn huu ndio ushauri wangu.
Kwa msaada ktk masuala Engineering/Installation of Beverages machines mnakaribishwa pm.
Ahsante.
 
Reactions: amu
Kuanzisha kiwanda ushauri unaomba huku?siulipe wataalamu wakushushie data halisi!! Huku tunadiscuss uchuuzi chuuzi ...maviwanda na pesa unayo nendea wataalamu!!
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…