Naomba ushauri kuhusu kununua gari

Naomba ushauri kuhusu kununua gari

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
Habari wandugu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, Nina uhitaji sana wa usafiri na nimefanikiwa kupata milioni 4 hivyo nataka kununua gari.Kuna magari mengi naona yanapostiwa mitandaoni kama vile ist,vitz,starlet,passo n.k

Yapo ya namba tofauti ila mengi yanaanzia C kurudi nyuma.Je kuna mwenye uzoefu wa haya magari ya kununua mtandaoni/madalali (kiuhalisia mengi ni bei rahisi).Je yanachangamoto gani? Mambo gani muhimu ya kuzingatia?

Binafsi ningependa gari zuri la kudumu nalo muda mrefu japo bajeti inanizuia lakini kwa muda huu ningependa nipate gari zuri ambalo halitonisumbua kwa bajeti niliyonayo.

Nitangulize shukrani kwa maoni yenu.
 
Utapata Ila yanakuwa na changamoto kiasi na kwa ushauri tu kutafuta gari LA mkononi lazima uwe na uvumilivu wa kutafuta

Mimi nimenunua gari used kwa m7 ya Izz namba B nimetumia m 1 kurekebisha na kukaa sawa

Ila siyo kanuni kila ukinunua gari kwa mtu linakuwa na changamoto mengine yapo poa kabisa pia OGOPA MADALALI na kuwa MVUMILIVU kwenye kutafuta

USIJE NUNUA PASSO
 
Utapata Ila yanakuwa na changamoto kiasi na kwa ushauri tu kutafuta gari LA mkononi lazima uwe na uvumilivu wa kutafuta...
Nimekuelewa sana na shukrani sana kwa maoni yako. Nikiri kwamba nimeshafanya udadisi muda mrefu mitandaoni kwa kulinganisha bei.

Pia ni bora wewe umejua milioni 1 imetosha kufanya matengenezo lakini mwisho wa siku gari bado iko njema kuliko kununua kisha baada ya muda inakufa jumla! Ila hapo kwenye Passo sijakuelewa mkuu!
 
Nimekuelewa sana na shukrani sana kwa maoni yako.Nikiri kwamba nimeshafanya udadisi muda mrefu mitandaoni kwa kulinganisha bei. Pia ni bora wewe umejua milioni 1 imetosha kufanya matengenezo lakini mwisho wa siku gari bado iko njema kuliko kununua kisha baada ya muda inakufa jumla! Ila hapo kwenye passo sijakuelewa mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Passo ya milion 4 itakuuwa Kwa pressure kumbuka wewe bado unategemewa na familia yako
 
Habari wandugu,

Niende moja kwa moja kwenye mada, Nina uhitaji sana wa usafiri na nimefanikiwa kupata milioni 4 hivyo nataka kununua gari.Kuna magari mengi naona yanapostiwa mitandaoni kama vile ist,vitz,starlet,passo n.k

Yapo ya namba tofauti ila mengi yanaanzia C kurudi nyuma.Je kuna mwenye uzoefu wa haya magari ya kununua mtandaoni/madalali (kiuhalisia mengi ni bei rahisi).Je yanachangamoto gani? Mambo gani muhimu ya kuzingatia?

Binafsi ningependa gari zuri la kudumu nalo muda mrefu japo bajeti inanizuia lakini kwa muda huu ningependa nipate gari zuri ambalo halitonisumbua kwa bajeti niliyonayo.

Nitangulize shukrani kwa maoni yenu.
Katika hayo yote uliyoyataja,achana na Passo na Vitz..... Ukipata Starlet au IST walau. Kama unafundi unamjua umshirikishe sana vinginevyo pesa yako utaitupa tu.
 
Nimekuelewa sana na shukrani sana kwa maoni yako. Nikiri kwamba nimeshafanya udadisi muda mrefu mitandaoni kwa kulinganisha bei.

Pia ni bora wewe umejua milioni 1 imetosha kufanya matengenezo lakini mwisho wa siku gari bado iko njema kuliko kununua kisha baada ya muda inakufa jumla! Ila hapo kwenye Passo sijakuelewa mkuu!
Nakushauri kama pesa yako ni tia maji tia maji kama Mimi tafuta gari kama ist,spacio,Carina ti na nyingine za sample hizo .UKISOMA SAMA HAPA JUKWAANI UTAJIFUNZA MENGI SANA KUHUSU MAGARI .
Pia gari unayotaka kununua Luna mambo mengi ya kuangalia unanunua kwa ajili gani ,he una mpango wa kuliuza badae kidogo ili ununue jingine ,na maswali kedekede mfano unampango wa kuliuza badae lazima uangalie umaarufu wa gari husika na upatikanaji wa spare
 
Back
Top Bottom