Naomba ushauri kuhusu matumizi ya nondo katika ujenzi wa ghorofa

Naomba ushauri kuhusu matumizi ya nondo katika ujenzi wa ghorofa

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
421
Reaction score
1,289
Nina rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya gorofa moja, katika mchoro wa ramani architecture aliweka kua zitumike nondo za 14mm beam na 16mm columms.

Katika kuanza kujenga fundi chuma alishauri kua floor moja haina uzito sana wakutisha kujengwa na nondo kubwa hivo yeye akasema ili kupunguza bei ya hesabu ya nondo aweke 12mm kwenye 16mm na 10mm kwenye 14mm.


Eneo analojenga liko tambarare (flat) na ni mchanga hivo sio ardhi ya kupasuka. Wiki hii kuna Eng Mchina alikuja nae saiti ambae ndio amesema atakua eng wake mchina akasema hakuna haja ya nondo kabisa za nguzo (beam) sehem za nguzo amimine zege lilikorogwa vizuri halafu nondo ataweka 8mm na 10mm kwenye slab na ngazi tu, tulitembelea baadhi ya site ambazo wamejenga hivo Magomeni floor 3 na Salasala floor 2 bila kua na nguzo zenye nondo ndani yake.

Kwa wataalam naomba ushauri
1. Tufate architecture alichosema
2. Ushauri wa fundi Chuma
3. Au Mchina ambae ni Engineer
 
Bora uingie gharama kwa kufuata ushauri wa fundi chuma ili uwe umefanya kitu cha uhakika kuliko kutokuweka nondo kabisa,

Huko ulipoenda kutembelea huenda ardhi yake ni tofauti na hapo kwako,

Au unaweza kuendelea kupata ushauri kwa maengineer wengine pia zaidi ya hao watatu.
 
Aangale mahesabu yanasemaje na kibali cha ujenzi kimepitishwa kwa michoro upi.

Sidhani kama machina yupo sawaa.
 
Architect yuko sawa. Tena kwenye kila column ziwe nondo za 16mm sita au nane na kwa beam 14mm ziwe sita vertical
 
Inauma sana Tanzania mambo yanavyo fanyika.

Kujibu swali lako.

Usifwate hata mmoja.

Nikianza huyo architect, je inakuaje architect anashauri mambo ya nondo na zege? Toka lini architect akawa STRUCTURAL ENGINEER? Architect jukumu lake ni kuchora ramani ya jengo full stop!! Mambo ya nondo yana wataalamu wao!! Alafu anasema uweke nondo za 14mm Tz kuna hizi nondo kweli?

Nikija kwa huyo fundi.

Anasema kwenye 16mm anaweka 12mm kwanini? Kwanini aweke 12mm na sio 10mm? Huyu ni fundi je ujuzi wa kusanifu majengo na kuchagua nondo za kujengea katoa wapi?

Haya nirudi kwa huyo mchina.

Kwanza ni engineer wa nini? Maana sio kila injinia ni mtaalamu wa majengo!

Anasema usiweke nondo kwenye beam kwanini? Na ametumia kigezo gani kusema usiweke nondo kwenye beam?

Kusema kuna nyumba walijenga bila nondo sio kigezo cha wewe kutotumia nondo! Unajua ni sababu gani wao walijenga bila nondo?

Kwa kukusaidia tu unaposemea beam unasema structural member inayo kuwa subjected kwenye tensional na compressional forces.

Na ujue tunatumia nondo sio kwa fashion au kwa sababu tuna ela ni kwa sababu tunajua zege ni weak ikiwa kwenye tension force na ndio maana tunaweka nondo ili atleast iiongezee nguvu beam hasa ikiwa kwenye tension!

Sasa huyo mchina wako analijua hili kweli? Ujenge beam ya ghorofa bila nondo si kutafuta kifo mchana kweupe?

USHAURI:

1. Lazima tufike sehemu tujifunze kutathimini taaluma za watu.

2. Tafuta structural engineer aku dizainie nondo na zege kwa ajili ya jengo lako. Ku size nondo za jengo sio jukumu la architect wala la fundi ni jukumu la STRUCTURAL ENGINEER.

3. Ukileta ubahili kwenye ubora jiandae baada ya miaka mitatu kuziba ufa kama sio kuzika watu watakao ishi ndani ya hilo jengo lenye beam zisizo na nondo.

Kila la heri.
 
Architect yuko sawa. Tena kwenye kila column ziwe nondo za 16mm sita au nane na kwa beam 14mm ziwe sita vertical
Ushauri wa maswala ya afya tunauchukua kutoka kwa daktari na sio mwanasheria. Vivyo hivyo ushauri wa nondo gani itumike tunauchukua kutoka kwa STRUCTURAL ENGINEER na sio ARCHITECT wala fundi.

Mpaka hapa huo ushauri wa architect ni ushauri usio faa kufwatwa maana hilo sio eneo lake kitaaluma.
 
Ushauri wa maswala tunauchukua kutoka kwa daktari na sio mwanasheria. Vivyo hivyo ushauri wa nondo gani itumike tunauchukua kutoka kwa STRUCTURAL ENGINEER na sio ARCHITECT wala fundi.

Mpaka hapa huo ushauri wa architect ni ushauri usio faa kufwatwa maana hilo sio eneo lake kitaaluma.
Nakubali boss uko sawa kabisa
 
Nina rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya gorofa moja, katika mchoro wa ramani architecture aliweka kua zitumike nondo za 14mm beam na 16mm columms...
Mwambie huyo mchina na fundi wake na huyo Architect wakupe calculations ambazo zimewaongoza kusema hivyo.

Halafu ndugu yangu ghorofa hazijengwi kienyeji hivyo. Una BOQ? Ulipewa kibali cha ujenzi kweli?

Usihatarishe maisha yako na ya wengine kisa saving.

Mwisho: Sio kila mchina ni Engineer ndugu. Ngozi nyeupe isikudanganye.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Uyo mchina nae Ni takataka TU.

Unajengaje beam bila nondo bhana?
 
Kwanini kwenye slab atumie 12mm na sio 10mm?
Inategemea na garama,pia wanashauri uzito wa chuma usiwe mzito sana...
Ila kwa utaalamu;
Example: We have to find the steel quantity for the room , Which size is 5 m x 4 m .

Given Data :


Size of Room = 5 x 4 meters

Main bars diameter = d = 12 mm

Distribution bars diameter = d =10 mm

Solution :

Spacing of Main bars = c/c = 15 cm c/c

Formula to find the No’s of ( M.B ) Main bars = 500 / 15 + 1= 34.33 say 35

Straight bar = 18

Bent up bars = 17

2) Spacing of Distribution bars = c/c = 20 cm c/c

Formula to find the No’s of ( D.B ) Distribution bars = 400 / 20 + 1= 21 No’s
 
This is a joke! Alafu unasema wanashauri je wanashauri akina nani? Unaposema uzito wa chuma usiwe mziti una maanisha nini? Na kwanini usiwe mzito?

Hivi mkuu unaelewa ulichoandika kweli? Embu tufike sehemu tuionee huruma fani ya uhandisi. Watu kama nyie ndio mnasababisha sekta ya uhandisi Tz iendelee kuto thaminiwa.

Narudia tena kusema mambo ya kihandisi waachiwe wahandisi.
 
Inauma sana Tz mambo yanavyo fanyika...

Kujibu swali lako...
Nimefaidika na ulichoandika.ki ukweli wengi hatujui kuwatofautisha achitects ,structrual Eng.na Quantity surveyor.

hapa tunahitaji elimu ya namna hii kwa kweli.Ndiyo maana majengo mengi yanaminyufa nyufa na mengine kudondoka.Yaani bongo ujenge nyumba isipasuke ufa ni nadra sana.

Halafu ubahili na tamaa ndiyo vinatu-cost mtu budget ndogo unataka ghorofa ya nini.
 
This is a joke! Alafu unasema wanashauri je wanashauri akina nani? Unaposema uzito wa chuma usiwe mziti una maanisha nini? Na kwanini usiwe mzito?...
Mkuu nadhani una complicate mambo kwa kiasi fulani.

Pamoja na kuwa wahandisi ndiyo kisheria wanaotakiwa kukadiria structural components, bado hiyo haizuii watu kujadiliana na kupata rough idea/estimates za materials yanayohitajika. Hii ni nyumba ndogo ambayo most likely itakuwa na live load ndogo, non-seismic flat sandy soil.

Roughly unaweza kupewa idea hata na civil engineer, masons, hata wajenzi waliojenga nyumba kama hizo kwenye udongo kama huo na hutokuwa mbali.

Kuna waezeka bati, wajenzi wa mitaani wanakupa estimates ambazo zipo almost perfect wakati vijana waliomaliza chuo kikuu huwa wanakuwa na errors kuliko wao. Hiyo ipo na inatokea.

Plus, kwa residential building ndogo kama inayozungumziwa hapa, wapo watu wajenzi kwa miaka karibu ishirini na wanakupa estimates nzuri tu. Na ukiwa unaweza kutumia softwares nzuri kama Staad Pro, unaweza kuja na designs nzuri tu na ukapata picha halisi au close enough.

Hii dunia sasa hivi, professing something hakuhitaji vyeti au kukaa shule. Ndio maana Elon Musk anakwambia college is for proving that you can do your chores.
 
Mkuu nadhani una complicate mambo kwa kiasi fulani.

Pamoja na kuwa wahandisi ndiyo kisheria wanaotakiwa kukadiria structural components, bado hiyo haizuii watu kujadiliana na kupata rough idea/estimates za materials yanayohitajika. Hii ni nyumba ndogo ambayo most likely itakuwa na live load ndogo, non-seismic flat sandy soil...
Hapa tunaongelea maisha ya watu wewe unasema nina complicate seriously?

Jengo la ghorofa unasema ni jengo dogo duuuh!

Naionea huruma sana hii nchi.
 
Hapa tunaongelea maisha ya watu wewe unasema nina complicate seriously?

Jengo la ghorofa unasema ni jengo dogo duuuh!

Naionea huruma sana hii nchi.
Anza kujionea huruma wewe kwanza. Kwa sababu hata hao ma engineer wa Tanzania hata Marekani sometimes hukosea na nyumba hubomoka.
Usipende kukariri.
 
Nina rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya gorofa moja, katika mchoro wa ramani architecture aliweka kua zitumike nondo za 14mm beam na 16mm columms.

Katika kuanza kujenga fundi chuma alishauri kua floor moja haina uzito sana wakutisha kujengwa na nondo kubwa hivo yeye akasema ili kupunguza bei ya hesabu ya nondo aweke 12mm kwenye 16mm na 10mm kwenye 14mm.


Eneo analojenga liko tambarare (flat) na ni mchanga hivo sio ardhi ya kupasuka. Wiki hii kuna Eng Mchina alikuja nae saiti ambae ndio amesema atakua eng wake mchina akasema hakuna haja ya nondo kabisa za nguzo (beam) sehem za nguzo amimine zege lilikorogwa vizuri halafu nondo ataweka 8mm na 10mm kwenye slab na ngazi tu, tulitembelea baadhi ya site ambazo wamejenga hivo Magomeni floor 3 na Salasala floor 2 bila kua na nguzo zenye nondo ndani yake.

Kwa wataalam naomba ushauri
1. Tufate architecture alichosema
2. Ushauri wa fundi Chuma
3. Au Mchina ambae ni Engineer
Mchina Siku zote NI mbana matumizi.

Architecture kazi yake mchoro tu.

Hapo mwenye ahueni kutokana na uzoefu wake ni fundi.

PIA HATA HAWA STRUCTURAL ENGINEER WA SIKU HIZI HAMNA KITU. ni watu wa kucopy na kupest.
 
Mchina Siku zote NI mbana matumizi.

Architecture kazi yake mchoro tu.

Hapo mwenye ahueni kutokana na uzoefu wake ni fundi.

PIA HATA HAWA STRUCTURAL ENGINEER WA SIKU HIZI HAMNA KITU. ni watu wa kucopy na kupest.
Ni bora structural engineer incase ikitokea shida unajua pa kumbana (ERB na vyombo vya sheria), fundi utampatia wapi?

NB: Ni architect na sio architecture, architect ni mtu architecture ni field.
 
Back
Top Bottom