Nina rafiki yangu anataka kujenga nyumba ya gorofa moja, katika mchoro wa ramani architecture aliweka kua zitumike nondo za 14mm beam na 16mm columms.
Katika kuanza kujenga fundi chuma alishauri kua floor moja haina uzito sana wakutisha kujengwa na nondo kubwa hivo yeye akasema ili kupunguza bei ya hesabu ya nondo aweke 12mm kwenye 16mm na 10mm kwenye 14mm.
Eneo analojenga liko tambarare (flat) na ni mchanga hivo sio ardhi ya kupasuka. Wiki hii kuna Eng Mchina alikuja nae saiti ambae ndio amesema atakua eng wake mchina akasema hakuna haja ya nondo kabisa za nguzo (beam) sehem za nguzo amimine zege lilikorogwa vizuri halafu nondo ataweka 8mm na 10mm kwenye slab na ngazi tu, tulitembelea baadhi ya site ambazo wamejenga hivo Magomeni floor 3 na Salasala floor 2 bila kua na nguzo zenye nondo ndani yake.
Kwa wataalam naomba ushauri
1. Tufate architecture alichosema
2. Ushauri wa fundi Chuma
3. Au Mchina ambae ni Engineer
Jambo la kwanza, uzito wa jengo haupimwi kwa macho bali kwa hesabu (na hapa utaangalia uzito wa jengo lenyewe tunauita self weight na uzito wa vitu vitakavyo kuwa ndani ya jengo).
Mbili, uchaguzi wa aina gani ya nondo zitumike hutegemea na kiwango cha mzigo ulio patikana wakati wa kufanya hesabu (structural analysis) na hivyo kiwango cha mzigo huamua size ya nondo na idadi ya nondo zitakazo tumika.
Tatu, izingatiwe kuwa kwenye soko hakuna nondo za 14mm, hivyo ushauri wa kutumia nondo za 14mm huonyesha wazi kuwa mshauri wa aina gani ya nondo zitumike sio mzoefu na mbobevu katika suala la ujenzi.
Nne, eneo la mchanga ni hatari pia maana mchanga unatabia ya kuhama napia mchanga hauna nguvu kubwa sana ya kuhimili mzigo (sand has low bearing capacity) hivyo umakini mkubwa unahitajika katika kufanya maamuzi.
Mwisho, kwa hali ya kawaida jengo la ghorofa moja litahitaji nondo za 16mm kwenye nguzo na beams, 12mm kwenye slab na 8mm kwenye ringi (stirrups/links).
Mpangilio wa nondo na idadi yake unategemea sana design ilivyo na analysis ilivyo pia.
Ushauri wangu, ikiwa hautojali waweza nitumia michoro ya Structure halafu nitakushauri cha kufanya, au waweza nitumia michoro ya architecture nii review then nitakushauri.
Ushauri ni bure tu wala usiwe na hofu b’se im you’re fellow Tanzania.
0621003092 is my WhatsApp number
Eng. Limbu from Limbu Nation Builders.