Naomba ushauri kuhusu matumizi ya nondo katika ujenzi wa ghorofa

Ndugu yangu uliyosema ni kweli. Lakini tujuwe mpja, huyo mjenzi asiye na vyeti kajenga chini za wenye vyeti kwa muda mrefu. Kwa hiy anajuwa mahitaji ya vifaa mbalimbali katikas ujenzi wa majengo mbali mbali. Ukimpa huyu fundi kazi anafuata kwa zoefu aliyoupata chini ya engineers. Kwa nondo atashauri kufuatana na alivyokuwa anaagizwa na mainjinia. Zege nalo anajuwa ni mifuko mingapi kwa mchanga kiasi gani na pia kwa kokoto kiasi gani bila kusahau size ya kokoto. So, this fundi is not doing things out of the air. He or she is following what he or she got from engineers worked with.
 
Hapo kuna mchoro ambao umepelekwa manispaa na ukapitishwa. Kwa hiyo huo mchoro umepitishwa na nani? Mpaka wapate permit.
Jambo la pili la kufikiria, Structural engineer anamrekebisha structural engineer mwenzake.

Kwahiyo uamuzi mzuri ni kufuata mchoro uliopitishwa na manispaa maana kama ulifuata taratibu zote basi bearing capacity ya udongo ishafanywa na mchoro wa nondo na zege ushafanywa na kupitishwa.

Sasa huyo engineer mwingine anatoka wapi? ... Yaani Mchina.

Ndiyo maana mimi naona ufuate mchoro, la sivyo msikilize fundi lazima atakuwa experienced na hao huwa wapo vizuri zaidi.
 
Kuna changamoto sana kuamini fundi au engineer kwa 100% kuna watu wanaweza kukufanyia vitu vya ajabu ndio maana unaambatana nao site, sio mbaya kuuliza ili kujiridhisha
 

Kama unataka kujenga nyumba yakichina mfuate mchina ndiyo maana vitu vya kichina vinahalibika haraka ila kama unahitaji kujenga ya imara na yauhakika fuata ushauri wa fundi chuma namm kuna chumba kimoja cha najenga bush ila nimejenga kwa kulaza tofauti nguzo nimetumia 12mm na slab nitatumia 12mm na 10mm
 
Jambo la kwanza, uzito wa jengo haupimwi kwa macho bali kwa hesabu (na hapa utaangalia uzito wa jengo lenyewe tunauita self weight na uzito wa vitu vitakavyo kuwa ndani ya jengo).

Mbili, uchaguzi wa aina gani ya nondo zitumike hutegemea na kiwango cha mzigo ulio patikana wakati wa kufanya hesabu (structural analysis) na hivyo kiwango cha mzigo huamua size ya nondo na idadi ya nondo zitakazo tumika.

Tatu, izingatiwe kuwa kwenye soko hakuna nondo za 14mm, hivyo ushauri wa kutumia nondo za 14mm huonyesha wazi kuwa mshauri wa aina gani ya nondo zitumike sio mzoefu na mbobevu katika suala la ujenzi.

Nne, eneo la mchanga ni hatari pia maana mchanga unatabia ya kuhama napia mchanga hauna nguvu kubwa sana ya kuhimili mzigo (sand has low bearing capacity) hivyo umakini mkubwa unahitajika katika kufanya maamuzi.

Mwisho, kwa hali ya kawaida jengo la ghorofa moja litahitaji nondo za 16mm kwenye nguzo na beams, 12mm kwenye slab na 8mm kwenye ringi (stirrups/links).

Mpangilio wa nondo na idadi yake unategemea sana design ilivyo na analysis ilivyo pia.

Ushauri wangu, ikiwa hautojali waweza nitumia michoro ya Structure halafu nitakushauri cha kufanya, au waweza nitumia michoro ya architecture nii review then nitakushauri.

Ushauri ni bure tu wala usiwe na hofu b’se im you’re fellow Tanzania.

0621003092 is my WhatsApp number

Eng. Limbu from Limbu Nation Builders.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…