mshana jr,
Asante Mshana, naomba kuongezea!,
- Gereji kuu ya kwanza ya Benzi ni DT Dobbie pale Nyerere Rd,
- Tatizo la DT Dobbie, hawatumii spear yoyote used, lazima ununue mpya!.
- Ushauri wangu, kama unaipenda benzi yako, na unajiweza kiuchumi, anzia DT Dobbie, watakupitishia kitu kinaitwa diagnostic machine, inakutolea print out ya kila ubovu wa gari lako.
- Baada ya hapo ndipo utapewa quotation ya DT Dobbie ujipime unaweza?!.
- Ukishindwa ndio sasa njoo hizi gereji za vichochoroni!.
- Vile vikolo kolo nenda duka la benzi pale kwenye jengo la Bilicans au used duka la Big D lindi Ste
Natumia E360, ilisumbua gear box, nikaanzia DT Dobbie, nikakuta vikolokolo kibao vibovu,
DT dobbie wakasema gear box wao hawafungui wala kutengeneza, bali wanakuagizia mpya toka Ujerumani kwa TZS. 8,000,000 na kuisafirisha TZS 1,500,000 kuifunga ni TZS.500,000 total ni 10 m!. Nikaona nyingi!,
nikashauri niende Mivinjeni kununua used, kwa TZS. 3,000,000, kuifunga TZS 200,000!. Huwezi amini, ndani ya miaka 6, nimebadili gear box mara 3, imenicost zaidi ya 10 m!, na sasa iko backyard the junk yard!.
Unaweza kusave kwenye used, ila in a long run ni maumivu makubwa zaidi!.
NB. Tusije kuanza kuitana mafisadi humu, hiyo Benzi sio gari yangu, ni gari ya wife wangu!, mimi usafiri wangu ninaomiliki ni boda boda!.
Pasco