mshana jr
Mkuu Mshana, DT Dobbie ni kweli wana bunya sana fingu, excuse yao ni genuine from Germany na wanaleta kwa DHL hivyo wanakamua sana!.
Niliwahi kuuliza headlight, hata kama imevunjika taa moja, unalazimishwa ununue set, kila taa 750,000/=, si nikaenda hapo kwa Big D, akanitolea hizo hizo genuine za Bosch kwa TZS. 500,000 pair, ila mwaka hazikumaliza zimeishaotesha ukungu!,
ndipo nikagundua jamaa anaagiza China, wanafanya copy cat hadi kuandika Bosch!, tofauti ile bosch genuine, maandishi yamevimba juu ya kioo, maandishi ya China, bosch imeandikwa kwa maandishi!, the funny part, ni genuine wanatumia crystal glass, mchina ni glass ya chupa ya kawaida, sasa mimi nilivyo bundi, mwaka haishi vioo ukungu!.
Sasa nimekuwa mzoefu nikiona hata kwa macho tuu, najua huyu mchini na hii ni genuine!. Ili kupoteza maboya, taa za benzi ukiziona ni clear glass ujue ni mchina!.
Hilo la kumiliki boda boda, si unajua tena wengine kazi zetu zinatulazimisha kuwa wajamaa, maana mwandishi kumiliki benzi, itambidi azidungulize sana haswa kwa kuzingatia vijibahasha vyenyewe vinatiwa 20,000 tuu!, ukipendelewa basi 50,000!, utavikusanya vingapi hadi vitoshe?.
Pasco.