Naomba ushauri kuhusu network market ya Neolife

Naomba ushauri kuhusu network market ya Neolife

Sim Card

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2019
Posts
881
Reaction score
1,601
Jamani naomba tu niwasalimu. Kuna changamoto moja naipata juu ya Neolife ni network market ambapo kuna mshikaji tunaheshimiana sana of course ni uncle ananilazimisha kujiunga nae. Anadiriki kunitukana kwamba utabaki maskini kama huoni fursa halafu pia yaani ananidharau.

Tatizo hata yeye sio kivile katoboa life sana japo pia sio poor kivile kwani ana hela ya kubadilisha mboga na nyumba mbili na vigari kama vitatu hivi.

Sasa changamoto hii networking hai-click kabisa kichwani kwangu, kwa jinsi bidhaa zilivyo na aina ya wateja inakuwa vigumu kwani ni lazima ujitangaze ili wanunue kwa jina lako upate points au uwaunganishe chini yako wanunue na kupanua mtandao ndipo ufaidi. For me naona ni ndoto.

Nimeamua kuwa quiet ili asinisumbue. Mungu ndio anapanga maisha ya mtu. Ushauri plse.
 
Hiyo kampuni iko vizuri na dawa zake ni za ukwel haswa na naiombea hiyo kampuni idumu sana na wasijebadilika Ila huko kwingine kwenye Mambo ya uwakala sijajua vzur japo nasikia wanajitahidi kulipa vzuri
 
Hizi ni pyramid schemes. Wachache wa juu ndo wanapata pesa. Wewe una uwezo wa kuwaunganisha watu wangapi nyuma yako? Kama una uwezo wa kuwaunganisha angalau watu 20 hivi nyuma yako ingia. Vinginevyo amua tu ujiunge ili kumfurahisha mjomba wako lakini siyo kwa lengo la kupata pesa.
 
Jamani naomba tu niwasalimu. Kuna changamoto moja naipata juu ya Neolife ni network market ambapo kuna mshikaji tunaheshimiana sana of course ni uncle ananilazimisha kujiunga nae. Anadiriki kunitukana kwamba utabaki maskini kama huoni fursa halafu pia yaani ananidharau.

Tatizo hata yeye sio kivile katoboa life sana japo pia sio poor kivile kwani ana hela ya kubadilisha mboga na nyumba mbili na vigari kama vitatu hivi.

Sasa changamoto hii networking hai-click kabisa kichwani kwangu,kwa jinsi bidhaa zilivyo na aina ya wateja inakuwa vigumu kwani ni lazima ujitangaze ili wanunue kwa jina lako upate points au uwaunganishe chini yako wanunue na kupanua mtandao ndipo ufaidi. For me naona ni ndoto.

Nimeamua kuwa quiet ili asinisumbue. Mungu ndio anapanga maisha ya mtu. Ushauri plse.
Kwanza hizo siyo dawa ni suppliments, pia haina tofauti na wengine kama akina Phyto science, tianshi, forever living, na wengine.. Wa juu ula wa chini huliwa , plus suppliments bei ghali ukichanganya na circle yako labda umezungukwa na watu wa kipato cha kati hawawzi kuafford basi jua ni kupoteza muda.
 
Mimi napata shida moja Sana ya uelelewa kwenye hii biashara. Sioni evidence za watu waliosaidika kwa kutumia hizi Suppliments na kupona magonjwa yao. Ila muda mwingi Sana naona Kuna kuhamasishana kuhusu kuingiza watu kwa ajili ya kulipwa mapesa na safari za nje etc. Inanitafakarisha Sana.
Mimi nilitumia za pid nikapona, shida ni moja hawaelezi ukweli kuwa dose mmoja haitatosha kukupa matokeo kwa sababu zile siyo dawa ni supplements, mimi nilipata mtu mkweli nikamweleza changamoto zangu alinijibu nitapona lakini lazima nijitahidi kuacha baadhi ya vyakula pia dose mmoja haitamaliza tatizo, nilitumia dose mfululizo miezi mitatu nikarudi hospital pid ikawa imeisha na baada ya miezi miwili Bwana Mungu alinifanyia kicheko ndani ya kizazi changu.
 
Kuna mtu ananipigia kelele nijiunge na eternal 🤔
 
Hata Mimi Nina ndugu yangu yupo Qnet huyo kila siku kunishawishi lakini kila nikifikiria bado haijaniingia akilini mpaka kesho kazi kunitumia sms za vijem eti Watu watakufa masikini ila mpaka muda yaani sijailewa
Mbongo akikuonesha fursa ujue wewe ndo fursa
 
Jamani naomba tu niwasalimu. Kuna changamoto moja naipata juu ya Neolife ni network market ambapo kuna mshikaji tunaheshimiana sana of course ni uncle ananilazimisha kujiunga nae. Anadiriki kunitukana kwamba utabaki maskini kama huoni fursa halafu pia yaani ananidharau.

Tatizo hata yeye sio kivile katoboa life sana japo pia sio poor kivile kwani ana hela ya kubadilisha mboga na nyumba mbili na vigari kama vitatu hivi.

Sasa changamoto hii networking hai-click kabisa kichwani kwangu, kwa jinsi bidhaa zilivyo na aina ya wateja inakuwa vigumu kwani ni lazima ujitangaze ili wanunue kwa jina lako upate points au uwaunganishe chini yako wanunue na kupanua mtandao ndipo ufaidi. For me naona ni ndoto.

Nimeamua kuwa quiet ili asinisumbue. Mungu ndio anapanga maisha ya mtu. Ushauri plse.
Nashangaa kuna watu huko wana vitambi vya hatari na wanauza virutubisho vya kuondoa vitambi/uzito.... hii imekaaje wakuu??
 
Mhh kuna mdada namjua aliishia diploma ya law eti na yy anajiita doc anaitibu sijui saratani sijui uvimbe..eti kwa hizo suppliments sijajua yy yupo kwny ipi..ila anakwambia ulete laki moja na nusu tuu umaskini utauaga...namwangalia kwny status zake..namcheki tuuu...
Halafu ukishawajibu hutaki wanakuchukia kabisa..sasa kama kweli hyo bness itanitajirisha nisipojiunga ww unachukia nini sasa...si uwaunge ukoo wako...
 
Kwanza hizo siyo dawa ni suppliments, pia haina tofauti na wengine kama akina Phyto science, tianshi, forever living, na wengine.. Wa juu ula wa chini huliwa , plus suppliments bei ghali ukichanganya na circle yako labda umezungukwa na watu wa kipato cha kati hawawzi kuafford basi jua ni kupoteza muda.
Umenikumbusha tiens mimi nilifanya nao tena nilikua wale watu wa mwanzo kabisa mkoani kwetu ipo hivi yule alie kuunga anapata pia kupitia wewe na yeyote utaemuunga chini yako pia kuhusu zawadi na safari ni uongo kutembea nchi mbalimbali kwa vikao na mikutano inajilipia everything ila lazima uwadanganye team yako ili wakaze buti watembee duniani magari wanayopewa ni uongo wanajinunulia then unaidanganya team yako umepewa zawadi niligundua nilipofikia level ya kuyajua haya.
 
Back
Top Bottom